MOSHI, KILIMANJARO
KOCHA wa Klabu ya Kilimanjaro FC ya mjini Moshi, Ally Chandika, amesema atahahakikisha timu yake inavuna pointi muhimu kutoka kwa vinara wa ligi daraja la Tatu, hatua ya sita bora, klabu ya Hai city ya wilayani Hai, katika mchezo wa kumalizia mzunguko wa kwanza, utakaopigwa kesho (Jumapili), kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, mara baada ya mazoezi ya klabu hiyo yanayofanyika katika uwanja wa Mandela-Pasua, Chandika amesema pamoja na changamoto zilizopo klabuni hapo vijana wake wako tayari kwa mchezo wa kesho hali inayochagizwa na ushindi wa 4-1 walioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Kilimanjaro.
Amesema pamoja na ugumu wa mchezo dhidi ya Hai city, ana uhakika wa kuondoka uwanjani na pointi tatu muhimu na kwamba tayari wachezaji wake ameshawaanda kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kutambua umuhimu wa kushinda mchezo huo kwa lengo la kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea mzunguko wa pili.
Kilimanjaro FC hadi sasa iko katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi zake saba baada ya kushuka dimbani mara huku Hai City wao wakijivunia kushika usukani wa msimamo wakiwa na pointi zao tisa.
Imetolewa na Ofisa Habari wa Kilimanjaro FC, Fadhili Athumani

No comments:
Post a Comment