Na Mwandishi Wetu
Benki ya Barclays
Tanzania imethibitishia umma wa watanzania ukuaji wake wa kasi wa teknolojia
kwa kuzindua huduma mpya na ya kisasa ya kuweka pesa kwenye mashine zake za ATMs
nchini.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa huduma
hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Uchuuzaji na Mikakati wa Benki hiyo, Bw Musa Kitoi alisema mashine hizo
za kisasa za i-ATMs zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na zina sifa ya
kipekee.
Alisema kwamba huduma
mbalimbali kama kuweka na kutoa fedha taslimu na hundi sasa zinaweza kufanyika
kupitia mashine hizo mpya na kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja wao.
Aliongeza kwamba benki
ya Barclays itaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wake kwa ufanisi wa
hali ya juu ikizingatia uhakiki wa huduma bora kwa wateja wake na kurahisisha
maisha yao kwa ujumla.
“Barclays tunawajali
wateja wetu na siku zote tunanuia kuwapa huduma za hali ya juu kufuatana na
matakwa yao, pia bidhaa na huduma zetu hupangwa kufuatana na mahitaji ya wateja
wetu,”
“Tunapenda
kuwathibitishia kwamba tuko katika kiwango cha juu sana kiteknolojia katika
soko na baadhi ya huduma zetu za kiteknolojia ya juu kama mfumo wa kutoa na
kuchukua fedha bila kujaza fomu, utumaji wa fedha kwenye mashine, benki kwa
njia ya simu na mwaka jana tumezindua service guarantee ikimaanisha uhakiki wa
huduma na kutimiza ahadi na kuwapa wateja huduma bora na za uhakika,” alisema.
Aliongeza kupitia mfumo
wao wa kidigitali wateja wao wanawezeshwa kujihudumia ili kujipatia muda wa
kutosha kufanya shughuli zao bila kupoteza muda wao mwingi kukaa benki.
Bw Kitoi alisema benki
ya Barclays itaendelea kuongoza katika soko kwa kutoa huduma bora na makini kwa
kutumia teknolojia ya hali ya juu.
Kwa upande wake, Meneja
Miradi na Mikakati wa Benki hiyo, Bi Jane Mbwilo alisema kwamba huduma hiyo ni
masaa 24 na mteja anaweza kuweka kiasi chochote kwenye mashine hizo za ATM hapa
nchini.
Alifafanua kwamba kwa
sasa mashine zipo 24 lakini wapo katika mkakati w mwisho kuongeza mashine hadi
kufika 30 katika maeneo kadhaa ya jijini la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment