HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 05, 2015

TAASISI 11 ZA KIISLAM KUSUSIA KURA ZA MAONI

Naibu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam na Shura ya Maimam, Rajab Katimba (kushoto) akitoa tamko la kuungana na taasisi 11 kupinga kuipigia kura Katiba inayopendekezwa. Kulia ni  Shekh, Hassan Abbas na Shekh, Juma Ramadhan. (Picha na Francis Dande)

TAASISI 11 za Kiislam zimesema zitasusia kura ya maoni ya Katiba pendekezwa kutokana na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya madhehebu ya dini, ikiwemo Maaskofu kuhusu muswada wa Makama ya Kadhi

Baadhi ya Taasisi hizo zinazopinga upotoshani ni Tampro, Basuta, Jasuta, IPC, Haiyat Ulamaa ma Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na Shura ya Maimamu ambazo zote hizo zimesajiliwa na zenye uwakilishi na mtandao wa kitaifa.

Upotoshaji huo, unalenga baadhi ya maoni yaliyotolewa na Waislamu, kupitia Jumuiya na Taasisi zao kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria yanayohusu mahakama ya kadhi kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Januari 19 mwaka huu.

Naibu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam na Shura ya Maimam, Rajab Katimba, amesema hayo wakati alipokuwa akitoa Tamko la taasisi hizo 11, linapinga waislamu kusemewa na taasisi zisizo kuwa na ridhaa ya waislam wote nchini.

Aliema, upotoshaji uliyowafanya wafikie hatua hiyo ni kauli zinazosema kuwa Taasisi hizo 11 zinawakilisha maoni ya wachache na ya wahab.

“Ukweli ni kwamba hoja hii inadhihirisha hofu ya mshikamano wa asasi za kiislamu katika kukubaliana na suala la mahakama hiyo ya kadhi.

“Ndio maana baadala ya kujibu hoja na maendekezo yaliotolewa na asasi hizi, matamko hayo yamejikita kwenye kushambulia taasisi husika kwa hoja ambazo zina misingi ya kuwagawa waislamu,”alisema Katimba.

Aidha, madai kuwa Muft ndiye mkuu wa Waislamu hapa nchini na kwamba ndiye anaye stahili kuteua makadhi nchini, taasisi hizo 11 wanayona madai hayo sio sahihi.

Alifafanua kwa kusema kuwa inawezekana kwa taasisi kuwa na muundo wa uongozi ambao unamfanya Mufti kuwa kiongozi  mkuu wa Waisilam wa taasisi hiyo na hapa Mufti atakuwa mkuu wa taasisi husika na sio Waislam wote nchini.

“Mfano wa taasi ambazo kiongozi wake mkuu ni Mufti ni Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) na sio kiongozi wa waislam wote nchini kama inavyodaiwa,”alisema Katimba.

Akizungumzia viongozi wa dini ambao sio Waislam mfano maaskofu ambao wametoa matamko ya kupinga Mahakama hiyo kwa hoja kuwa italeta hukumu za kukata mikono wasio kuwa waislam na kuwabagua.

Katimba alisema kuwa hoja hizo zote hazina ukweli na watoaji wa hoja hizo wanajua ukweli kuwa mahakama ya kadhi inayokusudiwa ni mahakama itakayotumia sheria za kiislamu ambazo zinatumiaka katika mahakama za kawaida tangu enzi za ukoloni mpaka leo.

Alisema inajulikana wazi kuwa mahakama ya kadhi itashughulika na mambo binafsi ya watu kwa mujibu wa sheria za kiislamu ambazo ni sehemu ya sheria halali zinazotumika hapa nchini.

Katimba, alisema mfano mambo hayo ni ndoa, talaka, mirathi, wakfu na malezi ya watoto hivyo, basi kinachofanywa na viongozi hao wa dini wasiokuwa waislamu ni kuivunjia heshima jamii ya kiislamu na kupotosha ukweli ambao uko wazi.

Aidha taasisi, hizo zimetaka serikali kusitisha mchakato huo wa kura ya maoni hadi pale suala la kadhi litakapo patiwa ufumbuzi kwani Waislamu hawapendezwi kwa suala hilo kuhusishwa na siasa hususani kuletwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu.

Alisema wakiendelea na mchakato huo wa kura ya maoni wataendelea na msimamo wao wakuisusia kama walivyofanya wakati wa Sensa ambapo matokeo yake yanajulikana kwamba ili feli. 

No comments:

Post a Comment

Pages