Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na maandalizi ya
tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wa Taifa. Sehemu ya
mapato ya tamasha hilo yatatumika kununulia baiskeli 100 kwa ajili ya watu
wenye ulemavu. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wa Taifa. Sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatatumika kununulia baiskeli 100 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya
Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam inayoratibu tamasha la Pasaka ambalo
mwaka huu linatarajiwa kutikisa mikoa 17, imepanga kutumia sehemu ya fedha za
kiingilio kununua baiskeli 100 kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu.
Hayo
yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama wakati akielezea
maandalizi ya Tamasha hilo ambalo litakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15
tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 katika kuutangaza utukufu wa Mungu.
Alisema
baiskeli hizo 100 zitagawanywa katika mikoa 10 na kutoa wito kwa wadau wa
muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika mikoa mbalimbali ambako tamasha
hilo litafanyika likipambwa na waimbaji mahiri kutoka ndani na nje ya nchi.
Msama alisema
utoaji wa baiskeli hizo za walemavu ni mwendelezo wa moja ya malengo ya tamasha
hilo ambapo ni kusaidia makundi maalumu katika jamii na kuongeza baada ya hapo kufanikisha
hili, wataangalia nini wafanye dhidi ya makundi mengine.
Kuhusu
waimbaji, Msama amesema kamati yake kwa sasa ipo katika hatua ya mwisho ya
mazungumzo na waimbaji mbalimbali wa kimataifa hasa kutoka nchini Afrika Kusini
na Uingereza ambako mazungumzo yanakwenda vizuri.
Aliwataja
waiombaji wanaofanya nao mazungumzo ni Solly Mahlangu, Rebecca Malope, Kekeletso
Foofolo na wengineo kutoka nchini humo kwa lengo la kuja kupamba tukio hilo la
maadhimisho ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.
Msama
aliongeza kuwa, hadi sasa wamepata maombi ya mikoa 17 wakitaka tamasha hilo
liwafikie, hivyo wanachoafanya sasa ni kufanya uchambuzi kuona mikoa gani
wanaweza kuifikia kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo mazingira halisi ya
kijiografia na kifedha.
“ Hoja si kupendekezwa
au kuombwa tu na wadau, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo
ya matamasha,” alisema Msama.
Aliitaja
mikoa iliyoomba Tamasha hilo ni Morogoro, Rukwa, Mara, Singida, Arusha,
Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora,
Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment