Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) Mart
Nooj, ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini kujiandaa na
mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika uwanja wa CCM
Kirumba jijin Mwanza Machi 29, 2015.
Taifa Stars inayotarajia kucheza na The Flames mwishoni mwa
mwezi huu, itaingia kambini machi 22 machi
katika hotel ya Tansoma kujiandaa na mchezo huo kabla ya kuelekea jijini
Mwanza machi 24 kwa maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo.
Wachezaji walioitwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo
ni; Magolikipa, Deogratius Munish
(Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Shomari Kapombe,
Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa
Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na
Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha
Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo
(Stand United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar),
Saimon Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu,
Mbwana Samatta (Tp Mazembe - Congo DR), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio
(Zesco United - Zambia)
Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza
machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka
la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA
Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na
kushika nafasi ya 100.
MARSH KUAGWA LEO MUHIMBILI Rais wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Mh. Jamal Malinzi ametuma salamu za ramirambi
kwa familia ya Marsh kufuatia kifo cha kocha wa Taifa ya vijana Sylvester Marsh
kilichotokea jana jijini Dar es salaam
Katika salam zake
kwa familia ya marehemu, Mh. Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini
TFF imeshtushwa na msiba huo na kusema Shirikisho na Taifa limempoteza mtu muhimu
katika mpira wa miguu nchini.
Mwili wa marehem
Marsh utaagwa leo saa 6 kamili mchana, katika kanisa la Hospital ya Taifa Muhimbili
na kutasafirishwa kuelekea Igoma jijini Mwanza kwa mazishi majira ya saa 8
kamili mchana kwa bus dogo (coaster) laTFF.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment