HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 15, 2015

OBRIGADO KUTUA TAMASHA LA PASAKA 2015

Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na ujio wa mwimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Thori Mahlangu (Obrigado). (Picha Francis Dande)
 Msama akifafanua jambo.
 
Na Loveness Mboje

RAIA  wa Afrika Kusini ambaye ni Mwanamziki wa nyimbo za injili, Thori Mahlangu (Obrigado), amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza katika Tamasha Pasaka litakalofanyika Aprili 5.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema kuwa sambamba na mwimbaji huyo ataambatana na waimbaji wengine 16 kutoka nchini humo huku Faustine Munishi maarufu kwa jina la Malebo na Solomon Mukubwa  kutoka nchini Kenya nao watakuwepo.

Msama alisema kuwa viingilio vya tamasha hilo kwa watoto vitakuwa shs. 2,000 viti vya kawaida shs.5,000 VIP B, shs. 10000 VIP A shs. 20,000 kwa watu wakubwa na kuongeza kuwa mara baada ya tamasha hilo, Aprili 12 itakuwa ni zamu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika Uwanja wa  CCM Kirumba.

Aidha kwa upande wa waimbaji wazawa  Msama amesema kuwa mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye alikuwa mwimbaji wa Upendo Group  naye atapamba tamasha hilo ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki.

Tamasha hilo linatimiza miaka 15 tangu lianzishe
na linatarajiwa kihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Afrika Kusini Uingereza na wenyeji Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages