Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Khamis
Pembe, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex
Msama. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
NA LOVENESS
BERNARD
KAMATI
ya Tamasha la Pasaka, imewahakikishia usalama wapenzi wa muziki wa Injili na
Watanzania kwa jumla katika tamasha hilo
litakalokata utepe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Mjumbe wa Kamati hiyo, Khamis Pembe,
alisema tayari wamewasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Kamishna (CP), Suleiman Kova.
Alisema
maandalizi ya Tamasha la Pasaka yamekamilika asilimia 90 na mwaka huu litakuwa
la aina yake.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alex Msama, alisema mwaka huu tamasha
linaadhimisha miaka 15 tangu lianzishwe na wanatarajia kumwalika Rais mstaafu
wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujumuika nao, kwani ndiye alikuwa mgeni
rasmi wakati linaanzishwa.
Msama
aliwataja waimbaji wengine watakaokuwepo katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na
John Lisu na Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama huku wakiwa katika mazungumzo na
mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Rose Muhando, kutokana na maombi ya wapenzi
wengi wa tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment