Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha kubwa la kuiombea amani nchi litakalofanyika Okroba 4.
(Picha na Francis Dande)
NA FRANCIS DANDE
KAMPUNI ya Msama
Promotions imeandaa Tamasha kubwa la kihistoria ambalo halijawahi kufanyika nchini
la kuiombea Tanzania
inayoelekea katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama Tamasha hilo
litafanyika Oktoba 4, jijini Dar es
Salaam.
Msama alisema kutokana
na uzito na heshima ya tamasha hilo,
linatarajia kushirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili wa ndani na
nje ya nchi ambao wanaotamba katika tasnia ya muziki huo.
Alisema japo ni
mara ya kwanza kwa kampuni yake kuandaa tamasha kama hilo katika historia ya uchaguzi nchini,
anaamini kwa vile amani ni kitu muhimu katiika uchaguzi, wengi watamuunga
mkono.
Msama alisema
anaamini wengi watajitokeza kuungana pamoja na viongozi wa kitaifa na kada
mbalimbali kuuombea uchaguzi huo ambao ni njia ya kidemokrasia ya kupata
viongozi kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani.
“Watanzania
wajiandae kuiombea amani Tanzania
kupitia muziki wa Injili hasa waimbaji mbalimbali wa kutoka nje ya Tanzania watashiriki katika tukio hilo ambalo bado tuko
katika mchakato wa mahali tutakapofanyia,” alisema Msama na kuongeza:
“Tamasha hilo kubwa kimaudhui
linakaribia Tamasha kubwa la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka tangu mwaka
2000,” alisema Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili.
Aidha Msama
alisema baada ya tamasha hilo kufanyika jijini
Dar es Salaam, watahamishia maombi hayo katika majiji mengine manne kwa lengo hilo la kuombea amani na
utulivu uchaguzi Mkuu.
Alitaja nchi
watakazotoka waimbaji watakaosindikiza maombi hayo ni
Afrika Kusini, Rwanda, Kenya, Uganda,
Zambia, Burundi na DR Congo.
No comments:
Post a Comment