Kamanda wa Kikosi Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (kulia)
akimkabidhi zawadi ya gari aina ya Toyota Sarf, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar
es salaam, Jackson Kapongo aliyeshinda kupitia mchezo wa Matumizi bora ya
Mitandao ya Kijamii iliyoendeshwa na Kampuni ya Enhance Auto ya Jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt. Picha na Father Kidevu Blog.
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt akionesha stika za kuhamasisha usalama barabarani ambazo pia zilizinduliwa na Kamanda Mpinga.
Meneja Mauzo Enhance Auto, Ayaka Kashida akionesha shindano jipya ambalo mshindi atajishindia Toyota Noah mpya.
Jackson Kapongo akiwa katika gari yake Toyota Sarf na pembeni yake ni Kamanda Mpinga.
Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia tukio hilo.
Bahati na sibu ilichezeshwa na wateja kujishindia mipira
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butta akitoa maelezo ya bahati nasibu ya kushinda mipira.
Na Father Kidevu
MHITIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson
Kapongo ameibuka mshindi na kukabidhiwa gari aina ya Toyota surf lenye thamani
ya zaidi ya sh milioni 24 katika shindano lililochezeshwa na kampuni ya kuuza
magari ya Enhance Auto.
Kapongo alikabidhiwa gari lake hilo na Kamanda wa
Polisi Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga baada ya kushinda katika shindano
lililoendeshwa na Enhance Auto likiwataka washiriki kuonesha ni namna gani
wanaweza kutumia mitandao ya kijamii na kujiletea manufaa.
Akizungumza kampuni hiyo, Mpinga alisema imekuwa
ikichezesha shindano hilo kila mwaka na kushirikisha nchi mbalimbali Afrika
ambapo kwa mwaka jana mshindi alipatikana kutoka Zambia lakini kwa mwaka huu
ameshinda mtanzania hivyo ni jambo la kujivunia.
Alisema mbali na kutoa zawadi lakini kampuni hizo
za magari zinajukumu kubwa la kutoa mchango kwa usalama barabarani kwa kutoa elimu
sambamba na kuuza magari yenye viwango vinavyokubalika ili kuepusha ajali
zisizo za lazima.
"Natoa wito kwa kampuni zingine kuwekeza
katika usalama barabarani na wasifikirie tu kuuza magari bali wahakikishe
magari yanakuwa salama na wanaoendesha wanakuwa salama... tuagize magari yenye
viwango mana ajali nyingi pia zinasababishwa na ubovu wa magari" alisema.
Mapema Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq
Butt alisema shindano hilo mshiriki anatakiwa kushiriki kwa kuchagua mitandao
yao ya kijamii kwa wingi zaidi na lilishirikisha nchi ambazo wanafanya nao
biashara ikiwemo Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Malawi, Msumbiji, Sudan
ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.
Hata hivyo alisema kwa kutambua umuhimu wa usalama
barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha Usalama
Barabarani wameanzisha kampeni ya 'Endesha kwa Usalama' ambapo pia
walikabidhi stika za magari lengo likiwa ni kujenga uhusiano na wateja wao.
Akizungumza zawadi hiyo, Kapongo aliishukuru
kampuni hiyo na kuwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa faida na si kwa
kujifunza mambo ambayo huharibu maadili ya jamii.
No comments:
Post a Comment