Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),
Dk. Naomi Katunzi akizungumza katika hafla ya kupokea madawati 1,000 kutoka
Kampuni ya Mafuta ya Total iliyofanyika mjini Bagamoyo. Jumla ya Shule 10 za
Msingi kutoka katika mikoa ya Pwani na Dar esSalaam zitanufaika na msaada huo. (Picha na Francis Dande)
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya
akizungumza katika hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya
Total, Jean-Christian Bergeron kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 1,000.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (wa pili kulia) akikata
utepe na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total, Jean-Christian Bergeron (wa tatu
kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 1000 yaliyotolewa kama msaada na
Total kwa ajili ya Shule 10 za Msingi kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akimshukuru Makamu wa Rais wa Kampuni ya
Total, Jean-Christian Bergeron baada ya kupokea sehemu ya msaada wa madawati
1000 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya Shule 10 za Msingi za mikoa ya Dar
es Salaam na Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika wilayani Bagamoyo jana. Katikati
ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nianjema, Ramadhan Hassan.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akiwa amekaa
katika madawati yaliyotolewa kama msaada na Kampuni ya Total. Katikati ni
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total, Jean-Christian Bergeron, madawati 1000
yaliyotolewa na kampuni hiyo yakiwa na thamani ya shs. milioni 78 kwa ajili ya
Shule 10 za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Wa pili kushoto ni
mwanafunzi wa shule ya msingi Nianjema ya Bagamoyo, Ramadhani Issa.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya akiwa amekaa
katika madawati yaliyotolewa kama msaada na Kampuni ya Total.
Naibu Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total, Jean-Christian Bergeron
pamoja na walimu wa shule za msingi za mkoa wa Pwani na Dar es Salaam baada ya
kupokea msaada wa madawati 1,000 yaliyotolewa na kampuni hiyo yakiwa na thamani
ya shs. milioni 78.
Picha ya pamoja.
Bagamoyo, Tanzania
Bagamoyo, Tanzania
SERIKALI imesema itawafukuza kazi walimu wakuu wa
shule zote za msingi ambazo wanafunzi wake watashindwa kusoma, kuandika na
kuhesabu kabla ya kuingia darasa la tatu.
Tamko hilo la serikali lilitolewa mjini Bagamoyo Mkoa
wa Pwani na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
mhandisi Stella Manyanya wakati akipokea msaada wa madawati 1,000 kutoka kwa
kampuni ya mafuta ya Total yatakayosambazwa katika shule 10 za mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, naibu waziri huyo
alisema ili kuwa na elimu bora katika hatua za awali lazima wanafunzi kuanzia
ngazi ya chekechea wajue kuhesabu, kusoma na kuandika kwa viwango vyao huku
akisisitiza kwamba kabla ya mwanafunzi kuingia darasa la tatu lazima kusoma,
kuandika, kuhesabu na kuelewa anachokifanya.
“Ni fedhaha unamkuta mwanafunzi wa darasa la tatu
hajui kusoma kwa nini? Lazima kuna uzembe mahali sasa hili ni agizo na
utekelezaji wake unaanza… tutapita huko kwenye mashule kukagua hili, tukibaini
wapo wanafunzi hawajui hizi KKK hatuna sababu ya kuednelea na huyo mwalimu
mkuu.
“…Tutamwambia atupishe akafanye shughuli nyingine,
lazima walimu wawajibike,” alisema Injinia Manyanya baada ya kuwapa karatasi
wasome na kuhesabu baadhi ya watoto wa shule za msingi waliokuwepo kwenye hafla
hiyo na kusema elimu bora ni pamoja na kujua kusoma, kuandika, kuhesabu na
kuelewa.
Naibu Waziri huyo pia aliipongeza Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA), kwa kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia katika elimu hasa
suala la madawati, ujenzi wa mabweni huku akisema taifa lina upungufu wa
madawati 1,349,090 ambayo gharama yake ni sh bilioni 182.1 hivyo aliwaomba
wadau wa elimu kuchangia.
Akizungumza kabla ya kukabidhi madawati hayo, Makamu
wa rais wa Kampuni ya Mafuta ya Total, Jean-Christian Bergeron alisema gharama
ya madawati hayo ni sh milioni 78 huku akibainisha kwamba kwa miaka mitatu
kampuni yake imechangia madawati 3,000 yenye tahamani ya sh milioni 234 ambapo
wanafunzi 9,000 wamenufaika nayo.
No comments:
Post a Comment