Mkurugenzi Mkuu wa Benki M,
Jacqueline Woiso akionyesha kifaa maalum kitakachochukua taswira ya hundi na kutuma benki popote ulipo, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Money moja kwa moja jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Bidhaa wa Benki M, John Brighton akfafanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Money moja kwa moja jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Bidhaa wa Benki M, John Brighton akfafanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Money moja kwa moja jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Jacqueline Woiso.
Mkuu wa Bidhaa wa Benki M,
John Brighton akionyesha kifaa maalum kitakachochukua taswira ya hundi na
kutuma benki popote ulipo, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Money
moja kwa moja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki M,
Jacqueline Woiso.
BAADA ya Benki Kuu ya Tanzania kuboresha huduma ya malipo kwa njia ya hundi, benki M imekuja na mfumo utakaopunguza foleni katika benki barani Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa bank hiyo Jacqueline Woiso alisema huduma hiyo ya Money.Moja kwa moja itasaidia kupunguza msongamano.
“Wateja wataepuka foleni za barabarani na hawatakuwa na muda wa kukimbizana kuwahi bank kabla hazijafungwa”alisema Woiso.
Alisema wateja wanaweza kufanya miamala ya hundi wakati wowote na muda wowote kwani mashine hizo wamezisambaza kwa wahusika wake.
“Money.Moja kwa moja ni huduma yenye usalama zaidi inayotumia mtandao wa intaneti ambapo mteja ataweka hundi kwenye kifaamaalum na taswira ya hundu na kutuma moja kwa moja bank”alisema Woiso.
Alisema kwa kufanya hivyo fedha hizo zitaingizwa kwenye akaunti zao bila wasiwasi wowote.
No comments:
Post a Comment