Upatikanaji wa jezi na vifaa vya Simba wasogezwa
karibu
Klabu ya Simba leo imeanza rasmi utekelezaji wa
kampeni yake ya uuzwaji wa jezi pamoja na vifaa mbalimbali venye chapa ya
Simba, ikiwa na dhumuni la kukuza mapato kwa timu kwa kupitia wanachama na wadau
wa Simba kununua bidhaa mbalimbali zenye chapa ya Simba, kupeleka huduma ya
vifaa vinavyotolewa na duka rasmi la Simba karibu zaidi na wanachama na wapenzi
wa Simba. Katika zoezi hili ambalo utaweza kununua jezi kwa Tsh. 15, 000/=
ambapo yoyote atakaenunua atapata picha kubwa ya timu bure.
Kwenye mechi na watani wa jadi wetu Yanga siku ya
Jumamosi, kikosi cha Simba kitavaa jezi nyeupe ambazo zitakuwa zikipatikana
kwenye duka la Simba linalotembea katika mitaa mbalimbali yaani Mobile Shop.
Akizungumza na Simba Sports.co.tz leo asubuhi wakati
zoezi hili lilipoanza Rais wa Simba Evans Aveva alisema “ leo tunaanza rasmi
zoezi letu la kutembea mtaa kwa mtaa kwenye kampeni yetu ya uuzwaji wa jezi
pamoja na vifaa mbalimbali venye chapa ya Simba kwa kutumia duka linalotembea “Mobile
Shop” zoezi hili ni maalumu kwa ajili ya kusogeza upatikanaji wa vifaa na jezi
za Simba kwa karibu zaidi, lakini pia itahamasisha wanachama na wapenzi wa
Simba kuchangia timu yao”
Tunatambua kwamba wanachama na wapenzi wa Simba
waliopo mikoni wangependa zoezi hili lifike na mikoani na punde tu tutakuwa na utaratibu wa jinsi
Duka letu la Simba Sports Shop litakavyoweza kupeleka huduma katika mikoa
mbalimbali Tanzania, aliongeza Rais wa Simba Evans Aveva.
Akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG Group Imani
Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya masoko ya klabu ya Simba
alisema “zoezi hili litakuwa endelevu ambapo tutaendelea kubuni njia mbalimbali
za kuwafikia watu waliopo mikoani nje ya Dar es Salaam ambapo kwa sasa wanaweza
kupata jezi rasmi ya Simba kwenye duka mtandao la Simba kupitia Jumia www.jumia.co.tz na jezi zitawafikia popote
walipo Tanzania”.
Simbasports.co.tz inaupongeza uongozi wa Simba SC
pamoja na wasimamizi wa Duka la Simba Simba Sports Shop kwa ubunifu huu katika
kuleta maendeleo ya klabu ya Simba.
No comments:
Post a Comment