NA
KENNETH NGELESI, MBEYA
JUMLA
ya shilingi bilioni 188.8 zimekuwa zikipotea kila mwaka kutokana na vipimo vya
Lumbesa kati ya hizo bilioni 14.8 serikali
imekuwa ikipoteza kama mapato ya kodi huku wakulima nchini kote wakipata hasara
ya zaidi ya sh Bilioni 174 kila mwaka.
Taarifa hiyo imetolewa na Dk. Goodluck Urassa wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,
Shule Kuu ya Biashara katika Mkutano wa wadau wa sekta ya biashara na kilimo katika
Ukanda wa kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) ulifanyika hivi
karibuni jijini Mbeya kwa kushirikiana na taasisi zingine nyeti nchini vikiwemo
baadhi ya vyuo Vikuu.
Akifafanua
zaidi Dk. Urassa alisema tafiti zilizofanywa kwa kupitia mpango huo mwaka 2012
tulifanya utafiti wa vipimo vya mahindi na mpunga walibaini serikali na wakulima
wenyewe wanapoteza fedha nyingi kwasababu ya ujazo huo wa ziada maarufu kama
lumbesa.
Dk.
Urassa alisema kutokana na hali hiyo wameanzisha mtandao utakao tafiti kero za
kibiashara na kilimo katika mikoa hiyo na kuziwakilisha serikalini ili
zifanyiwe kazi na kwamba serikali inakila sababu ya kuboresha mazingira ya
biashara bna kilimo ili kutanue wigo wa ajira nchini.
Alisema
kwa kupitia mpango huo ujulikanao kwa jina la (BEST) ambayo umelenga kuboresha
mazingira ya biashara nchini utasaidia kuibua mambo mbalimbali yanayoongeza
kero kwa wafanyabiashara na wakulima na kufanya utetezi.
“Tunashughulikia
mambo ya kodi za mazao, vipimo, bidhaa feki, pembejeo feki. Tunafanya utafiti,
tunatoa mafunzo na tunatoa ushauri na kufanya mazungumzo na serikali ili
kuiboresha sekta hii ya biashara,” alisema Dk. Urassa
Alisema
kuwa kuna utafiti mwingine unaoendelea kufanyika katika Mkoa wa Njombe juu ya matumizi
ya pembejeo feki na athari ambazo serikali na wakulima wanapata ambapo matokeo yake yatatolewa Februal mwaka.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa mtandao wa Multi Actors Integration (MAI), Lucas
Mwakabungu alisema kuwa wadau hao kuwa ni pamoja na Chemba ya Wafanyabiashara,
wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) ya mikoa ya Iringa, Morogoro, Mbeya, Njombe na
Ruvuma ambayo yote ipo katika ukanda huo wa ujulikao kwa jina la (SAGCOT)
Katika hatua nyingine Mwakabunga
alibainisha taasisi
zingine zilizopo katika mtandao huo kuwa ni pamoja na Umoja wa Vyuo Vikuu
Nchini, vyombo vya habari na washirika wengine katika sekta ya biashara na
kilimo likiwemo Jukwaa la Wadau wa Kilimo Tanzania (ANSAF), taasisi
inayojihusisha na kilimo cha mbogamboga, matunda na maua nchini (TAHA) na
mpango wa SAGCOT wenyewe.
Alisema
kwa kupitia ufadhili wa shirika la (BEST AC) mpango huo ni wa majaribio na
umefanyiwa tafiti wa mwaka mmoja katika mikoa hiyo, na kwamba utafanywa pia
katika mikoa mingine ili kuoanisha matokeo yake.
Mwakabungu
alisema wadau hao watakaokutana mara mbili kwa mwaka wataongozwa na wawakilishi
kutoka umoja wa vyuo vikuu kufanya utafiti huo na kutoa ushauri wa kuondoa
vikwazo vya biashara serikalini ili iweze kuboresha mazingira mazuri ya
biashara.
Mkutano
huo ambao ulifanyika kwa muda wa siku mbili na jijini Mbeya ili kuainisha
baadhi ya kero zinazoigusa sekta ya biashara na bada ya kuziainish,Kero hizo
zitapelekwa katika vyuo vikuu ambavyo vimeshiriki zifanyiwe utafiti kabla ya
kupelekwa serikalini kwa ajili ya kuzishughulikia.
Alizitaja
baadhi ya kero hizo ambazo ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya biashara na
wafanyabiashara wenyewe kuwa ni pamoja na wingi na ukubwa wa kodi na mikopo
yenye riba kubwa.
Mwakabungu
alisema utafiti wao wa awali unaonesha katika biashara moja nchini kuna kodi
zaidi ya 20 huku wenye viwanda wakirundikiwa kodi zaidi ya 30 kwa mwaka jambo
linalopunguza idadi ya walipa kodi badala ya kuongeza wigo wa walipa kodi.
No comments:
Post a Comment