Na Bryceson Mathias,
Mvomero.
MENEJA wa Kiwanda cha
Sukari Mtibwa, raia wa Afrika kusini, Greg Swart, na Meneja wa Fedha, wamewakimbia
wafanyakazi wa Kiwanda hicho wanaodai Mshahara wa Mwezi Januari, baada ya
Kufunga Milango yote ya kiwandani hapo.
Awali Uongozi wa Kiwanda
hicho, ulitangaza kwenye Mbao za Matangazo kwamba, Mshahara huo utalipwa, Februari
13, jambo ambalo wafanyakazi hawakukubaliana kwa tarehe hizo wanatakiwa kulipwa
Mshahara wa Kati (half payment).
Kutokana na sintofahamu
hiyo, Diwani wa Kata ya Mtibwa, Luka Mwakambaya (Chadema), amewasiliana na Mkuu wa Wilaya,
Betty Mkwasa, ili aende akawatatulie tatizo hilo Sugu (amekubali), ambalo
wafanyakazi na wananchi wa eneo hilo wanaliita Donda Ndugu.
Kinachowatesa Wafanyakazi
na Wananchi wa Kata ya Mtibwa, Meneja Swart, amekuwa Mwiba wa Uchungu kwao, kabla
na baada ya kurejea tangu alipofukuzwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete,
Septemba 7, 2010, kwa kutumia
lugha chafu za matusi na za kudhalilisha wananchi, hasa waajiriwa.
Akiwa
Kiwanda cha Sukari Mtibwa, na Wazee wa Mji Mdogo wa Madizini, Septemba
7, 2010, Kikwete alimwagiza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Mvomero, Fatma Mwasa, sasa Mkuu wa Mkoa Geita, kukutana na makundi
yanayohusika
yakiwemo ya menejimenti na ya wakulima wa miwa.
Kufukuzwa kazi nchini kwa Meneja huyo raia wa Afrika Kusini,
kulitokea baada ya Raisi Kikwete kufika Mtibwa,
Turiani wilayani Mvomero mkoani Morogoro, akiwa katika mikutano yake ya
kampeni, ambapo alielezwa na Wananchi kero na matatizo yanayowakabili dhidi ya
uongozi wa Kiwanda hicho.
Wakati wananchi wakiwa hawajaridhishwa na kurejeshwa kwake
kinyemela, bado mioyo yao imeanguka kutokana na kuona, licha ya Mneja huyo
kurejea kinyemela, bado hajajifunza na kujirekebisha makosa ya awali, na
wanaishangaa Uhamiaji Meneja huyo kuwepo nchini.
No comments:
Post a Comment