RAIS DK.MAGUFULI |
Akizungumza Baada ya Kukutana na
Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo, Balozi Huyo, Dianna Melrose
Amesema Juhudi za Mapambano dhidi ya ufisadi pamoja na kubana matumizi na ubadhirifu wa mali za umma kunakotekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Awamu ya
Tano ni mfano wa kuigwa.
Balozi Melrose amesema Waziri Mkuu wa nchi ya Uingereza, David Cmeroon amevutiwa na Utendaji kazi wa Rais
Magufuli na kusisitiza kwamba nchi hiyo itaendeleza ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Uingereza na Tanzania Katika Nyanja Mbalimbali Za
Maendeleo.
Kabla Ya Kukutana Na Balozi Wa
Uingereza Hapa Nchini Rais Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Balozi
Wa Afrika Ya Kusini Hapa Nchini Mh Thamsanqa Mseleku,Na Balozi Wa Misri Hapa
Nchini Mh Mohamed Yasser El Shawaf Ambao Amewahakikishia Kuwa Serikali Yake Ya
Awamu Ya Tano Itaendeleza Ushirikiano Mzuri Uliopo Kati Yake Na Nchi Hizo
Hususani Katika Kukuza Biashara Na Kuwanufaisha Wananchi Wa Pande Zote.
Katika Hatua Nyingine Rais Magufuli
Amepokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wawili.
Mabalozi Waliokabidhi Hati Zao Za
Utambulisho Ikulu Jijini Dar Es Salaam Ni Mh Jean Pierre Mutamba Tshampanga Wa
Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Mh Theresia Samaria Wa Namibia.
Rais Magufuli Amewaeleza Mabalozi Hao
Kuwa Tanzania Itaendelea kushirikiana Na Nchi Hizo Katika Nyanja Mbalimbali
Hususani Katika Uchumi.
Wakati Huo Huo Rais Wa Jamhuri Ya
Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na
Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar Es
Salaam.
No comments:
Post a Comment