Balozi mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nchini Tanzania (DRC) Pierre Mutamba amewataka Wakongomani waishio nchini Tanzania kuwa na umoja na kufanyakazi kwa bidii ili waweze kujenga nchi yao, amesema hayo wakati Balozi huyo akianza kazi rasmi, leo katika ofisi za Ubalozi huo zilizopo Upanga jijini Dar es salaam.
Balozi Mutamba amewaambia wanajumuia hao kuwa falsafa yake ni “Ni hapa kazi tu” inayofuata nyayo za Kauli Mbiu ya Rais John Pombe Magufuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi Mutamba alitoa Bendera za Taifa lake kwa kila Kiongozi wa jumuia ya Wakongomani waishio hapa nchini ikiwa ni ishara ya Uzalendo wa Taifa lao, Balozi huyo alisema kuwa Bendera ni Nembo ya Nchi, kwa hiyo ni jukumu la kila Mkongomani kuijenga nchi yake.
Wakongomani waishio hapa nchini walimundalia Balozi Mutamba hafra fupi ya kumkaribisha kufanya kazi hapa nchini, hafra hiyo ilifanyika katika ofisi za Ubalozini huo. Viongozi wa jumuia mbalimbali za Wakongomani hao wamesifu uteuzi wa Rais Joseph Kabila wa kumteua Balozi Mutamba hapa nchini, kwani uwakilishi wake umewapa matumaini, kwa jinsi Balozi huyo alivyochukua hatua ya haraka kufungua milango kwa Wakongo wote waishio hapa nchini ubalozini hapo kushirikiana naye kudumisha uhusiano wa nchi hiyo na Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii.
Naye Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (BCI) waishio hapa nchini Mukendi Kabobu amehaidi kuwa wafanyabiashara wa chama hicho watampa ushirikiano mkubwa Balozi huyo kuondoa kero zote zilizokuwa zikikwamisha shughuli zao. Rais wa chama cha hicho cha wafanyabiashara, amesema kuwa chama hicho kinafanya kazi pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania na wengine wakiwa wanachama wa chama hicho.
Kabobu amesifu utendaji wa Rais John Magufuri kwa kurekebisha mambo mengi kwa kipindi kifupi cha uongozi wake. Mwenyekiti wa wazee wa Kikongomani hapa nchini amemfananisha Balozi Pierre Mutamba na ‘Kichwa kizuri cha mashua’ ambaye atawavusha salama’ kwani Balozi huyo amekuja na falsafa ya kuwaunganisha pamoja Wakongo wote.
No comments:
Post a Comment