Na Talib Ussi, Zanzibar
Baada ya siku
,mbili za mjadala mkali ndani ya Baraza
Kuu la Taifa la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), leo linatarajiwa kutoa tamko
zito kuhusiana na mwelekeo wa siasa na usalama baada ya uchaguzi mkuu wa marejeo wa machi 20
mwaka huu.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti Twaha Taslima kinaeleza kuwa
mjadala ulikuwa mkali huku wajumbe wakiwa na maoni tofauti juu ya mustakabili
wa chama hicho pamoja na Zanzibar kwa ujumla.
“Kikao kikao kimekwenda vizuri mda kuu ni hali
ya siasa na usalama wan chi na leo tutatoa Baraza Kuu litatoa tamko juu ya hali
inavyo endelea” alisema Omari Ali Shehe ambaye ni mkurugenzi wa Uchaguzi na
Mipango.
Kikao hicho kiliaza
juzi mjini hapa na kushirikisha wajumbe wote wa bara na visiwani ili
kuzungumzia hali ya siasa na chama hicho pamoja uchaguzi wa kulazimishwa
uliofanyika wiki mbili zilizopita.
“Mtalezwa leo taarifa
yoote kwa hiyo kwa sasa niachie nisije kuvunja utaratibu” alisema Shehe
Baada ya uchaguzi huo
ambao ulimpa ushindi Dk. Ali Muhammed Shein vitendo kadhaa vimekuwa
vikiripotiwa ikiwemo baadhi ya watu kupigwa ovyo pamoja na uchomaji moto nyumba
na watu kuaza kufarakana unguja na Pemba.
Jeshi la Polisi
linanyoosha vidole baadhi ya wanasiasa kwa kuchochea vitendo ambavyo vinatishia
hali ya usalama wa nchi lakini wakati huo huo wananachi katika kisiwa cha
Tumbatu ambapo nyumba zao zilichomwa moto wiki iliyopita wanailaumu polisi kwa
kukupendelea Chama cha mapinduzi (CCM) katika kushuhulikia matokio ya uhalifu.
Tangu matokio hayo
kuaza kuripotiwa viongozi na wanachama wa
CUF Pekee ndio ambao wanakamatwa na Polisi na kuwekwa Korokoroni na
hakuna kiongozi wa CCM aliyekamatwa hata pale ambapo nyumba za wafuasiwa CUF
zimechomwa moto.
Fatma Khamis mwenye
watoto wa Nne mkazi wa kijiji cha chwaka Tumbatu wilaya ya kaskazini A Unguja alisema
alishtuka usingizini na kualazimika kukimbia baada ya watu wasiojuilikana na
kuvunja nyumba.
“Tulikimbia kwa kuokoa
maisha yetu kwani hatukujua wale walikuwa akina nani na lengo gani” alisema
fatma.
Fatma alisema watu
wengi wamekimbia eneo lao kutoka nyumba zao kutiwa alama ya X bila kujua ina
lengo gani.
No comments:
Post a Comment