Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga
akikata utepe wakati wa uzinduzi wa tawi la Asasi binafsi ya kusaidia sekta ya
kilimo Kanda ya Magharibi (PASS), katika
mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi ambapo itamwezesha mkulima kupata huduma za
kitaalam za maendeleo ya biashara na huduma za kifedha. Uzinduzi huo ulifanyika
mjini Kigoma, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya PASS, Andrew
Temu. (Na Mpigapicha Wetu)
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga
akizungumza na wajumbe wa bodi ya Asasi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo
Kanda ya Magharibi (PASS) mara baada ya kuzindua tawi la taasisi hiyo Kanda ya
Magharibi itakayohusisha mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi ambapo wakulima watapata huduma za kitaalam za
maendeleo ya biashara na huduma za kifedha. Uzinduzi huo ulifanyika mjini
Kigoma, mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya PASS, Andrew Temu.
No comments:
Post a Comment