HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 02, 2016

Hatimae Rais Magufuli ataja kiwango cha pesa anacholipwa kama mshahara wa Rais Tanzania

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli
Na Millard Ayo


Baada ya baadhi ya Wabunge wa vyama vya upinzani Tanzania kumtaka Rais Magufuli kuanika hadharani mshahara wake pamoja na makato ya kodi, Rais Magufuli ambaye ni Rais wa awamu ya tano kwenye Jamuhuri ya muungano wa Tanzania amekubali kuutaja mshahara wake.

Kama kawaida yake yeye ni shabiki wa kipindi cha TV cha Clouds 360 on CloudsTV ambacho alikipigia simu kwa suprise March 17 2016, sasa wakati anatazama kipindi hicho April 1 2016 akiwa nyumbani kwao Chato, Rais Magufuli akaona Watangazaji wakisoma magazeti na kukawa kuna habari moja kwamba Wabunge Zitto Kabwe na Tundu Lissu wanamtaka ataje kiwango cha mshahara anaolipwa kama rais wa Tanzania.

Muda mfupi baadae President aliwasiliana na Watangazaji wa Clouds360 na kusema mshahara wake ni shilingi za kitanzania MILIONI 9.5 na akasema yuko tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake na kutoa mchanganuo akimaliza mapumziko Mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment

Pages