May 16, 2016

ILO ZATOA MAFUNZO KWA MADAKTARI 380 JUU YA NAMNA YA KUTATHIMINI AJALI NA MAGONJWA YANAYOTOKANA NA KAZI

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba akielezea malengo ya Mfuko na kazi zake, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kwenye jengo la LAPF jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016. Mafunzo hayo yanalenga kuwaelimjsha madaktari namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
 
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanza kutua mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. Jumla ya madaktari 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo hayo.

Mafunzo yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.  Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dr. Jacques Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa kutokana na kazi. Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha, Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki.

Bw. Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata ajali au kuugua na wakapata ulemavu”
 Baadhi ya washiriki wa mafnzo wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, SSRA., Bi. Irene Isaka, akitoa hotuba ya ufunguzi
 Washiriki.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba.
 Bi. Isaka na Masha wakiwa kwenye meza kuu wakiandaa hotuba zao.
Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dkt. Jacques Pelletier (kulia) na Dkt. Sylvie Thibaudeau wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kutoa mada zao.
Afisa Mwandamizi wa WCF, Rehema Kabongo, akiwakaribisha washiriki na wageni wengine kwenye mafunzo hayo.
 Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya WCF, Bw. Athuman H. Msengi, akiwasili ukumbini huku akisaidiwa na msaidizi wake.

No comments:

Post a Comment

Pages