HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2016

Kikwete asaini Kitabu cha Maombolezo Ubalozi wa Kenya

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyeambatana na Mkewe, Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya hapa nchini kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya, Mhe. Nwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki kilichotokea wiki iliyopita nchini Uingereza. Mwingine katika picha ni Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Boniface Muhia. Dkt. Kikwete anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye mazishi ya Mama Kibaki yatakayofanyika Nairobi, Kenya. (Picha na Reginald Philip).

No comments:

Post a Comment

Pages