Mwishoni mwa wiki iliyopita Mfuko wa Pensheni wa LAPF ulidhamini Kongamano la Jeshi la Polisi (Vikosi vya masuala ya tiba) uliofanyika mjini Tabora.
Mfuko wa Pensheni wa LAPF ulitoa kiasi cha Shs. 6,200,000/= katika kufanikisha mkutano huo wa kujipima na kujadili changamoto mbalimbali za kitengo cha tiba ndani ya Jeshi la Polisi.
Wawakilishi kutoka mikoa yote Tanzania walishiriki katika kongamoano hilo wakiwa ni maofisa waandamizi wa jeshi hili la polisi. katika kongamano hilo Mfuko ulipata wasaa wa kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko lakini pia mada ya maandalizi kabla ya kustaafu ilitolewa, udhamini huu una synergy kubwa na mfuko katika kusajili wanachama wapya ndani ya jeshi la polisi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi ACP Paul Kasabago akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya TZS. 6,200,000/= iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni LAPF kuwezesha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania (medical wing) mjini Tabora. Wanaokabidhi kutoka LAPF ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama Bw. Valerian Mablangeti, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Desdery Sigonda pamoja na Meneja Kanda ya Dar es Salaam Bi. Amina Kassim.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa mada kuhusu Mfuko ikijumuisha maandalizi kabla ya kustaafu, Maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi wakisiliza kwa makini katika kongamano la jeshi hili lililofanyika mjini Tabora hivi karibuni.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakifuatilia kwa makini mada toka Mfuko wa Pensheni LAPF kwenye kongamano la Jeshi hili lililofanyika mjini Tabora ambapo maafisa hao walivutiwa na kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari ikiwa ni maandalizi kabla ya kustaafu
Mmoja ya Maafisa waandamizi walioshiriki kongamamo la jeshi la Polisi mkoani Tabora hivi karibuni akiuliza namna ya kujiunga kwa hiari na Mfuko wa Pensheni wa LAPF mara baada Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitoleawazo na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.
No comments:
Post a Comment