HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2016

Master Card Foundation yatoa dola milioni 10 kuimarisha kazi za ubunifu

NA GLORY CHACKY

SHIRIKA linalojihusisha na maendeleo vijijini (Master Card Foundation) limetoa dola za kimarekani  zaidi ya Miliomi 10.6 ili kuimarisha kazi za ubunifu  na kupunguza umaskini.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salam jana  na  Gabriel Kivuti Mtaalamu wa mambo ya kiufundi wakati wa kukabidhi tuzo kwa makampuni matano kutoka nchi nane  Barani Afrika.

Alizitaja kampuni zilizoshinda kuwa ni APA Insurance ltd, Finserve Africa LTD/equitel, M-KOPA LLC  ya Tanzania, Musoni Kenya ltd pamoja na Olam Uganda ltd.

“Kampuni hizi zilionyesha fikra za ubunifu kama mbinu za kupata fedha za kutosha,ongezeko la upatikanaji wa huduma kama akaunti za akiba, bima na mikopo”alisema
Alisema fedha hizo zitasaidia kuongeza wigo wa kifedha kwa takribani watu maskini milioni nane katika maeneo ya vijijini Afrika ikiwemo Tanzania,Kenya na Uganda.

Kwa upande wake Nick Hughes Mkuu wa bidhaa na mwanzilishi wa M-kopa  kutoka Tanzania alisema  fedha walizoshinda zitawasaidia wakulima kupata pembejeo za kilimo, nishati na huduma za kifedha.

Hata hivyo kulikuwa na ushindani mkubwa na makampuni mengi ambapo kampuni zilizoshinda zilionyesha nia ya kuleta mabadiliko ya kweli ya kifedha kwa watu maskini

No comments:

Post a Comment

Pages