Maria Inviolata
Kanda ya Mashariki, inayojumuisha mikoa ya Morogoro, Pwani na wenyeji Dar es salaam ilikamilisha mchakato wa kutafuta DJ bora anayechipukia kwa kutoa washindi wawili watakaoingia katika fainali za Kitaifa kumpata Dj bora 2016 anayechipukia. Mashindano ya kanda hiyo yalifanyika jana katika ukumbi wa Billicanas jijini Dar es salaam.
Walijitokeza washiriki 30 kutoka kanda hiyo ya Mashariki, washindi watatu walioingia raundi ya pili wote wanatoka mkoa wa Dar es salaa, washindi hao ni Dj Scruch Disigner(Kinondoni) Dj Sam TZ (Ukonga) na Dj Lonark kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Washindi walioingia mzunguko wa tatu ni Dj Disigner na Dj Lonark. Mshindi aliyetwaa ufalme wa kanda ya Mashariki ni Disigner, Hata hivyo shindano hilo lilikosa msisimko kutokana na washiriki kutokuwa viwango maalum vya shindano hilo.
Awali mashindano hayo yakianza Jaji Mkuu wa shindano hilo Dj Steve B hakuridhika na ushiriki wa Ma dj hao, kwani walijitokeza washiriki wachache licha ya shindano hilo kutangazwa kwa muda mrefu na kutoa viwango vinavyotakiwa kwa mshiriki kuwa navyo.
Mratibu wa Shindano hilo hilo Adam Mchomvu, lililoandaliwa na kituo cha Luninga cha Clouds alisema kuwa washindi wawili watakaoshinda shindano hilo la kanda ya Mashariki wataingia moja kwa moja katika mashindano ya Taifa ya kumpata DJ bora anayechipukia.
Mashindano hayo ya Kitaifa yatazishirikisha kanda zote zilizotoa washindi, mshindi wa Kitaifa atapata mashine mpya ya muziki “Pioneer”, shilingi milioni 2 na kupata nafasi kushiriki kwenye Fiesta nchi nzima.
Naye Jaji msaidizi wa shindano hilo la kanda ya Mashariki Dj Tass alitaja vigezo vitatu vya kumpata mshindi, vigezo hivyo ni kutumia kwa ufasaha mashine ya muziki, kuchanganya muziki, kuchezesha klaisti, utundu na uchangamfu wa kulimiliki jukwaa,
Hata hivyo washiriki wengi walioshiriki shindano hilo hawakuwa na vigezo vilivyotajwa ilihali wakilazimila kuomba msaada kwa wasidizi washindano hilo namnaya kutumia kompyuta ya kisasa aina Aplle ili kuchukua na kuupeleka muziki kwenye ‘Pioneer’.
Jambo hilo lilimsikitisha sana Jaji mkuu wa shindano hilo kuona wengi wa washiriki hao kuwa na uelewa mdogo wa kutumia mashine hizo.
Mwandishi wa Gazeti hili alipotaka ufafanuzi kutoka kwa Dj na mtangazaji maariufu Millard Ayo kuhusu uelewa mdogo ilioonyeshwa na washiriki wa shinda aliyekuwepo eneo la shindano ili kuwapa moyo washiriki Wa shindano hilo la “So so fresh Dj Compee”, Millard alisema kuwa mashine iliyotumika ni sawa na mashine zinazotumika hapa nchini, na kuongeza kuwa washiriki wengi wa shindano hilo hawakufanya mazoezi ya kutosha, Alisema mtangazaji huyo.
Jambo hilo lilithibitishwa na mmoja wa washiriki wa shindano hilo, aliyesema kuwa yeye alilisikia shindano hilo siku hiyo, hivyo hakujiandaa ingawa alipata nafasi ya kushiriki, hata hivyo mshiriki huyo ilibidi akiri wazi akiwa jukwaani kuwa hakujiandaa na kuruhusiwa kutelemka.
Hali hiyo ilimsikitisha zaidi Jaji Mkuu wa shindano hilo Dj Steve, aliyesema kuwa hakutemea washiriki wa shindano hilo kutoka Kanda hiyo hususan mkoa wa Dar es salaam kuwa na washiriki wachache tena wenye viwango vya chini kushiriki shindano hilo. “Dar mmeniangusha sana, nilitegemea kupata wakati mgumu wa kumpata mshindi wa kanda ya Mashariki kutokana na jiji la Dar kuwa kitovu cha kila kitu” alisema Dj Steve.
Akizungumzia mwenendo wa shindano hilo katika kanda nyingine , Dj Steve alisema mkoani kulikuwa na ushindani mkubwa sana kuliko ushindani duni ulioonyeshwa na jiji kuu la kibiashara yaani Dar es salaam.
Washindi wa shindano hilo la kanda ya Mashariki wote wamehaidi kufanya mazoezi zaidi kuhakikisha mfalme wa shindano hilo Kitaifa anatoka katika mkoa wa Dar es salaa.
Hakuna Dj wa kike alitejitokeza kushiriki shindano hilo la kanda ya Mashariki tofauti na kanda nyingine, alisema mratibu wa mashindano hayo ya kumpata Dj bora anayechipukia Kitaifa Dj Adam Mchomvu.
No comments:
Post a Comment