|
Wanahabari mkoa wa Iringa wakishiriki kufanya usafi katika soko la Manispaa ya Iringa leo |
Mwenyekiti wa matukio na maafa wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin (mwenye ndoo) akimwaga takataka katika dampo baada ya kuzizoa ndani ya soko kuu la Iringa wakati wa shughuli za usafi leo
|
Na MatukiodaimaBlog
WAKATI
leo ni maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani
kwa maadhimisho hayo kitaifa kufanyika mkoani Mwanza ,wanahabari
mkoa wa Iringa kuitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira
katika eneo la soko kuu la Manispaa ya Iringa.
Huku
wakiomba serikali kuangalia upya uamuzi wake wa kuzuia matangazo ya
moja kwa moja kutoka bungeni kuwa ni kuwakosesha wananchi kupata uhuru
wao wa kupata habari.
"
Huo ni uhuru wa kuzaliwa nao.sheria zote zinazotungwa zinapaswa
kuzingatia haki hiyo. Miaka 15 iliyopita tz ilikuwa na sheria 16
zinazominya uhuru wa habari, hivi sasa sheria hizo zimeongezeka hadi 26
na serikali iko mbioni kupeleka nyingine hivi karibuni. .....Wanahabari
na wadau wake tukikubali serikali iendelee kutuletea sheria za aina hiyo
tutakawa tunakubali kujenga ukuta wa kuzuia Upatikanaji na usambazaji
wa habari. ...tunaomba serikali izingatie maoni ya wadau wakati ikitunga
sheria hizo"
Mwenyekiti
wa kamati ya matukio na maafa wa chama cha waandishi wa habari
mkoa wa Iringa (IPC) Bw Francis Godwin alisema kuwa shughuli
hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 2.30 asubuhi hii kwa
wanahabari wote mjini Iringa kushiriki usafi kabla ya kuendelea na
majukumu yao ya kila siku.
Alisema
imekuwa ni kawaida ya wanahabari mkoa wa Iringa kufanya
maadhimisho hayo kwa aina tofauti tofauti ikiwemo ya kusaidia watu
wenye mazingira magumu ,kuchangia maendeleo ya mkoa huo upande wa
elimu na kuwa mwaka jana waliadhimisha siku hiyo kwa kutoa mifuko
ya saruji ya Tsh 500,000 kwa mkuu wa wilaya ya Iringa kwa ajili
yakuchangia ujenzi wa maabara .
Hata
hivyo alisema kwa kuwa wanahabari ni chachu ya maendeleo katika
jamii wataendelea kufanya shughuli mbali mbali za kijamii katika mkoa
wa Iringa na kuiomba jamii kujenga utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo yao.
Pia alisema ni vema Manispaa ya Iringa ama serikali ya mkoa kutunda sheria kali itakayowabana wananchi wanaotupa taka ovyo kwa kuwatoza faini kati ya Tsh 50,000 ama 100,000 ili kukomesha tabia hiyo.
Kwani alisema upo uwezekano wa kutoa ajira kwa vijana kuzunguka mitaani kukamata wanaochafua mazingira na kuwapeleka ofisi za mwanasheria wa Manispaa na kuwatoza faini na kama faini ni Tsh 50,000 basi kijana atakayekamata mchafuzi wa mazingira alipwe Tsh 30,000
Alisema
kuwa kauli mbinu ya maadhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo
vya habari ni UPATIKANAJI WA HABARI NI UHURU WA KIMSINGI ,HIVYO NI
HAKI YAKO
|
No comments:
Post a Comment