Na Mauwa Muhammed, Zanzibar
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema serikali iliyopo hivi sasa haiwezi kuongoza watu zaidi ya asilimi 80 walioikataa
Alisema kutokana na hilo alieleza kuwa wananchi kuigomea Serikali hiyo ni haki yao.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho na wapenzi katika ofisi ya Wilaya ya Mjini iliyopo Kilimahewa Mjini Zanzibar.
“ Ni haki yao wananchi kuchukua hatua ya kugomewa CCM kwani hawakuichagua katika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 25, 2015’’ alieleza Maalim Seif.
Alisema Serikali hivi sasa imekabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi pamoja na waziri wa fedha kutangaza kukusanya bilioni 8 kwani hawana uwezo wa kupata fedha hizo kwani wahisani wamezuwia misada yote.
Alisema njia ya mgomo baridi itamtoa Dk Shein katika madaraka kwani alidai kuwa si rais halali wa Zanzibar alipitwa kwa zaidi ya kura 25 elfu katika uchaguzi wa octo na mia nane haijapata kutokea katika chaguzo za Zanzibar tokea enzi ya ukoloni.
“Nilimpita kwa kura elfu 25 narudia kusema tena Simtambuwi na serikali yake sitashirikiana nayo “alisema maalim Seif
Alisema pamoja na kuwa wao wanatumia bunduki,mabomu lakini njia ya mgomo ndiyo itakayomtoa hatosita kudai haki yake mpaka haki itakaporejea.
Alisema chaguzi za nyuma alilazimika kunyamaza kwani alikosa ushahidi wa kutosha lakini kw mara hii ana ushahidi wa kutosha kwani ana matokeo ya uchaguzi ya kila kituturi vilivyofanyika uchaguzi wa Unguja na Pemba
“mara hii mpaka kieleweke na kitaeleweka watakamata watu wataleta mazombi lakini silaha pekee ni umja”alisema Maalim Seif.
Aidha alisema wito kuitwa kwake katika kituo cha polisi ni moja katika vitisho ambavyo amekuwa akifanyiwa ili aweze kurudi nyuma lakini ameapa hatorudi nyuma.
Maalim Seif ambae ni makamo wa kwanza msaafu amesema atafanya kazi ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha haki ya wananchi.
Ziara ya wilaya ya mjini ni muendelezo wa ziara za kutembelea chama chake katika wilaya zote za Unguja na Pemba.
No comments:
Post a Comment