Ratiba rasmi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
msimu wa 2016/2017, imetoka.
Ratiba hiyo imezingatia michuano mbalimbali ya
kitaifa na kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za taifa ili kukwepa dhana
yoyote ya upangaji wa matokeo na kurundikana kwa michezo.
Hii ni ratiba rasmi ukiachana na ile ambayo
ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Ile ya mitandao ya kijamii imekosewa anwani ya
Posta ya TFF kadhalika kuonesha kuwa mchezo kati ya Azam FC na African Lyon
ungefanyika Agosti 21, 2016 ilihali hii rasmi ina anwani sahihi na mchezo huo
wa raundi ya kwanza ukionesha utachezwa Agosti 20, 2016.
Tunaomba familia ya soka kuegemea kwenye hii ya
sasa rasmi inayotolewa na TFF.
…………………………………………………………....………… …………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA
MPIRA WA MIGUU TANZANIA



No comments:
Post a Comment