Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimakabidhi zawadi ya Laptop Macbook air, Shaffih Dauda baada ya kuibuka mshindi katika Shindano la 'Shinda na TemboCard'
NA IRENE MARK
MWANDISHI na
Mchambuzi wa masuala ya soka hapa nchini, Shaffih Dauda ameibuka kidedea katika
shindano la Shinda na Tembokadi linaloendeshwa na Benki ya CRDB.
Dauda ni
miongoni mwa washindi wanne wa Julai ambao ni wateja wa benki hiyo waliotumia
zaidi kadi zao katika kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.
Akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza washindi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa
CRDB, Dk. Charles Kimei shindano hilo limehamasisha matumizi ya tembokadi za
benki hiyo.
Dk. Kimei
aliwataja washindi ambao ni wateja wa benki hiyo kwa Julai kuwa ni Nasir
Mnkande aliyepata tiketi ya ndege kwenda Dubai pamoja na familia yake, Dauda
aliyeshinda Laptop Macbook air.
Aliwataja
washindi wengine ambao ni mawakala wa Fahari Huduma kuwa ni Benrad Swai aliyepata
Laptop Mackbook Air na kampuni ya Mzenzi Investment iliyopata Ipad air.
“Tunalenga
kuwavutia wateja wetu wengi zaidi ili waamini kwamba kufanya malipo kwa tembokadi
ni rahisi, nafuu na salama… mteja habebi fedha nyingi ni kadi yake na namba ya
siri tu.
“Mshindi ni
yule atakayekuwa amefanya mihamala mingi yaani amenunua bidhaa mbalimbali kwa
kuchanja kadi yake kwenye mashine za wauza bidhaa au huduma au kwa mwezi
husika,” alisema Dk. Kimei ambaye ni mtaalam wa shughuli za kibenki kimataifa.
Alisema shindano
hilo la miezi sita limeongeza mahitaji ya tembokadi hadi kufikia kadi milioni
1.6 na kusambaza vifaa vya manunuzi 1,500 kwa biashara na taasisi mbalimbali
hapa nchini.
Hata hivyo
walizawadiwa pia washindi wa Juni ambao ni Wakwetu General Supply na Deograsy
Mlay walionyakulia Laptop Mackbook air, Eunice Manamba aliyepata Ipad air na
Hassa Nyimbile aliyepata tiketi ya ndege kwenda Dubai na familia yake.
Shindano hilo
linaendelea huku wateja wa CRDB wakimasishwa kushiriki kwa kutumia Tembokadi
zao wanapofanya manunuzi ya gharama yoyote.


No comments:
Post a Comment