Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),
Joel Laurent, akizungumza na Wamiliki wa Shule na Vyuo visivyo vya serikali
(TAMONGSCO) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Nyasa katika mkutano uliofanyika
katika Ukumbi wa JKT jijjini Mbeya. Kulia ni Mwenyekiti Tamongsco Taifa,
Kitururu Mzava na Mwenyekiti Kanda, Asanga Ndile. (Picha na Kenneth Ngelesi)
NA KENNETH NGELESI, MBEYA
WAMILIKI na
mameja wa shule zisizo za Serikali hapa nchini TAMONGSCO wameshauriwa kuwapeleka
wakuu wa shule kushiriki semina na vikao mbalimbali vinavyo husiana na masuala
ya kitaalumu badala ya gharama za kumsafirisha walimu kmushiriki vikao hivyo.
Wito huo
ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Wamiliki na Maneja wa Vyuo na shule zisizo
za Serikali TAMONGSCO,kanda ya nyanda za
juu kusini Asanga Ndile baada ya kuona kuna idadi ndogo ya walimu wakuu na
wakuu wa shule ikilinganishwa na wamiliki na mameneja wa shule katika kikao.
Akizungumza
katika kikao cha dharura kilichofanyika juzi katika Bwalo la JKT katika Viwanja
vya Nane nane Ndile alisema kuwa kumekuwa na tabia ya wamiliki wa shule kuto
waruhusu walimu wakuu na wakuu shule na Vyuo, kushiriki vikao vya jumhiya hiyo
kwani wao ndiyo wanajukumu kubwa na kuinua kiwanngo cha elimu katika shule zao
badala ya wao na mameja wa shule ambao wengi wao hawana utaalamu katika masuala
ya elimu.
‘ Hili
nimeona katika kikao cha leo lakini pia hata kiliocho pita walioshiriki ni
wachache sana,na tulicho kiona wengi hawana taaluma ya ualimu sasa umuhimu wa
elimu hajui kuwa mwali8mu anatakiwa atumike zaidi sasa yeye anawaza
nimsafirishe huyu hawezi kurudi na pesa kumbe kule atarudi na utaalamu
uliondaliwa na tamongsco’ alisema
Alisema
ushiriki wa wawakuu wa shule katika semina,Mikutano na warsha hizo watarudi na
utalaamu wenye manufaa kwa ajili ya shule zao hivyo wanapaswa kuona umuhimu wa
kutuma wakuu wa shule kuudhuria vikao, semina na mikutano hasa zile zinahusiana
na masula ya kitaaluma.
Aidha Ndile
alisema kuwa hivi sasa wapo katika ushindani wa kutoa elimu bora hivyo ili
kukabiliana na hilo wanachama wake hawabudi kuwawwezesha wakuu wa shule kwani
bila hivyo shule walizojenga yatabaki magofu.
‘Ndugu
zangu tupo katika Ushindani kwanza sisi wenyewe lakini pia kuna ushindani na
shule za Serikali hivyo hanabudi kuwawezesha walimu wetu wakuu kitaalumu hasa
kushiriki Semina na Mikutano kama hii kwani wao ndiyo wataalumu na kuziwesha
shule zetu kuendelea kufanya vizuri’ aliongeza Ndile
Kwa upande
wake Mwenyuerkiti wa Jumuhiya hiyo taifa Kitururu Mzava alisema wakati wa
kulala kwa wanachama wake umepita kwani sera ya elimu bure ni changamoto kwao.
Alisema
kuwa hivi sasa Serikali imeanza kuboresha shule zake hivyo ni wakati mwafaka
kwa wamiliki binafsi kuamka na kufanya vizuri zaidi ili ziendelea kuwa kufanya
vizuri zaidi.



No comments:
Post a Comment