HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 14, 2016

BONANZA LA MWALIMU NYERERE ARUSHA LAFANA

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya (DAS), David Mwakiposa.
Katibu Tawala wilaya ya Arusha,David Mwakiposa akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,katikati ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akifatilia kwa makini na kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno .
Watoto wakichuana kukimbia mbio za mita 50 kwenye Bonanza hilo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro(wa pili kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa mchezo wa Karate mkoa wa Arusha,Richard Kitoro pamoja Sensei Dad na Sensei David wakifatilia michezo iliyokua ikiendelea.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice akionyesha umahiri wake kwenye mchezo wa Karate.
Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kushirikiana na wadau wa michezo pamoja na wananchi wa Jiji wameadhimisha siku ya Mwl. Nyerere kwa kuandaa na kushiriki kwenye Bonanza la Michezo lililopewa Jina la Bonaza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh  Amri  Abeid uliopo jijini hapa leo tarehe 14.10.2016. 



Tamasha hili limeandaliwa maalumu kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyenyere aliyefariki miaka kumi na saba iliyopita sambamba na kusherekea kilele cha Mwenge wa Uhuru ambao ulipita katika Wilaya ya Arusha mwishoni mwa mwezi wa nane na kuzindua miradi ya Afya, Maji, Elimu, Uwezeshaji wananchi, uwezeshaji makundi maalumu, Ujenzi na Usafi wa Mazingira yenye thamani ya zaidi ya TshBil 1.5.



Akiongea na wanamichezo walioshiriki katika Bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusa Mhe. Gabriel Fabian Daqarro alisema Tamasha hili ni kwa ajili ya kumuezi Mwl. Nyenyere ambapo litasaidia vijana na wananchi kuweka miili yao safi, kujiepusha na maradhi pamoja na makundi yanayoweza kusababisha kujiingiza kwenye madawa ya kulevya, ulevi na uzururaji.



Pia tuitumie siku hii kutafakari mafundisho na maelekezo ya Mwalimu Nyerere aliyoyatoa wakati wa uhai wake, wapi Nchi imetoka, Misingi imara ya Uongozi bora na namna gani tunaweza kuenenda ili kuleta maendeleo katika Taifa letu, na vijana kama nyie ndio mnaotakiwa kuwa chachu katika kupambana na umasikini katika Nchi yetu alisema Dc Daqarro.



Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Bw. David Mwakiposa alielezea Tamasha hilo kuwa limeshirikisha michezo mbalimbali kama Netball, Football, Volleyball, Basketball, mchezo wa Bao, kukimbiza kuku, Baiskel, kuvuta kamba, Karate, Taekondo, Uchoraji pamoja na riadha.


Bonaza hili pia limetumika kama jukwaa la kuendelea kuelimisha na kueneza ujumbe kwa vijana kupitia kauli mbiu ya Mwenge mwaka 2016 inayosema “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa washirikishwe na wawezeshwe”.

No comments:

Post a Comment

Pages