Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya
Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes
Quality Plaza, Dar es Salaam ambapo
Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wajasiriamali kuwafichua watendaji wa
mamlaka za kurasimisha biashara watakaowadai rushwa wakati wa kupatiwa huduma
ya kurasimisha biashira zao.
Makamu wa Rais alitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati kufungua
Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasirimali Tanzania (VoWET).
Alisema wanawake hawapaswi kuogopa kuwafichua watendaji
wanaowaomba rushwa kwani wanawakwamisha katika harakati zao (wanawake) za
kujiendeleza kibiashara,kiuchumi na pia kukwamisha juhudi za serikali katika kuinua
maendeleo ya Wanawake nchini.
Rais wa VoWET Bi. Maida Waziri (kulia) akihutubia wakati wa Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania ambapo licha ya kupongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika masuala mbali mbali ya kumuwezesha mwanamke pia alielezea changamoto ambazo wanawake wanakutana nazo katika shughuli zao za kuwainua kiuchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia baadhi ya kazi za ubunifu zilizofanywa na Wanawake Wajasiriamali kabla ya ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya
Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa PH Planes
Quality Plaza, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment