HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 26, 2016

MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MV TANGA KUZINGATIA USALAMA WA ABIRIA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa  Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko  Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA Tanga Bw. Lusenga David.


Na Theresia Mwami, TEMESA TANGA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa kivuko cha Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.

Amesema hayo alipotembelea na  kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga kinachosafiri kati ya Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya suala la usalama wa abiria na  kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato ya kivuko hicho.

Ndugu zangu hapa tunabeba roho za watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia” Alisisitiza Dkt Mgwatu.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko  Ngoroma amemuahakikishaia Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko vingine vilivyopo mkoani Tanga.

Aidha kwa upande wao watumishi wa Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

 Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages