HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2016

CWT MKOA WA DAR ES SALAAM YATOA MAFUNZO KWA MAOFISA ELIMU KATA

  Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Daar es Salaam (CWT), Abdallah Kaula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya mafunzo kwa maofisa Elimu Kata. (Picha na Francis Dande).
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Uluoch akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya mafunzo kwa maofisa Elimu Kata.  
 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Uluoch akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa maofisa Elimu Kata.  
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Uluoch akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa maofisa Elimu Kata.  
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Uluoch akitoa mada wakati wa semina ya mafunzo kwa maofisa Elimu Kata.  

NA HAPPINESS MNALE

CHAMA cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dar es Salaam kimesema jumla ya walimu 4769 wanaidai serikali zaidi ya sh. Bilioni tatu.

Fedha hizo zinatokana na malimbikizo ya madai mbalimbali yakiwemo ya waliopandishwa madaraja kutorekebishiwa mishahara yao, likizo,uhamisho, matibabu na posho ya kujikimu.

Akizungumza katika semina ya maofisa elimu wa Kata, Katibu wa CWT, Mkoa wa Dar es Salaam, kwa Abdallah Mkaula, alisema kwamba katika mwaka 2015/16 baadhi ya walimu walipanda madaraja na kurekebishiwa mishahara yao lakini kwenye uhakiki wa wafanyakazi hewa waliondolewa.

“Zoezi la kuhakiki wafanyakazi hewa lilipoanza walimu hawa 5,182 waliopandishwa madaraja waliondolewa mishahara yao mipya na hawajui hatima yao,”

“Wilaya wa Ilala walimu wa shule ya msingi wanaodai 303, Kinondoni 1499, Temeke 1678 kwa upande wa sekondari Ilala ni 725, Kinondoni 615 na Temeke 365,”alisema
Mkaula alisema kwamba walimu 4,414 wamefunguliwa wigo wa madaraja yao mwa 2015/16 lakini wengi wao hawajalipwa mishahara yao mpya.

“Walimu wa shule waliofunguliwa wigo wa madaraja kwa upande wa shule za msingi kwa Wilaya ya Ilala ni 1070, Kinondoni 1,660 na Temeke ni 1287 na kwa sekondari ni Ilala ni 215, Kinondoni 126 na Temeke 56,”alisema Mkaula

Aidha alisema kwamba walimu 488 wa shule za Msingi wilaya ya Ilala wanadai zaidi ya Sh. Milioni 216.
“Kwa walimu wa shule za msingi Kinondoni wanaodai ni 1721 zaidi ya Sh. milioni 660 na Temeke ni 2560 kiasi cha Sh. Bilioni 1.50,”

Kwa walimu wa sekondari Ilala wako 277 wanadai Sh. Milioni 126 na Temeke wako 1241 wanaodai zaidi ya Sh. Milioni 508,”alisema.

Mkaula alisema kwa upande wa walimu waliostaafu kazi mwaka 2015/16 hawajalipwa mafao yao ya kuwarudisha makwao.

“Walimu 148 kati yao wanadai fedha za kusafirishia mizigo zaidi ya Sh. Milioni 381 ambapo walimu 67 ni wa wilaya ya Temeke na 91 wa kinondoni ambao wanadai zaidi Sh. Milioni 228,”alisema.

Naye mwezeshaji wa semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu CWT, Ezekiah Uluoch, alisema kwamba kati mambo ambayo maofisa hao watafundishwa ni kufahamu haki, wajibu wao na vipengele vinavyowapa sifa.

Alisema pia watazungumza kuhusu hesabu za vyama zinavyokaguliwa, madai ya sheri mbalimbali na kuchukua maoni ili kuyafikisha kwa Rais John Magufuli aliyeahidi atakutana na viongozi wa chama cha walimu.

Aidha alisema kwamba semina hiyo pia inawajengea uwezo wa kutambua namna ya kuwaongoza na kuwasaidia walimu.

No comments:

Post a Comment

Pages