HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 30, 2016

NSSF KUTOA JIRA 3000


SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeamua kujikita katika uwekezaji wa viwanda na majengo ili lisitetereke kifedha na kushindwa kutoa huduma kwa wanachama wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, wakati wa kusaini makubaliano na atakayekuwa mwendeshaji wa hoteli ya Mzizima Towers alisema uwekezaji ni moja ya sekta muhimu katika mifuko ya jamii.

Alisema shirika hilo kwasasa lipo katika mchakato wa kusaidia ufufuaji wa kiwanda cha nafaka kitakachokuwa kikitengeneza unga.

Akizindua jengo hilo Kahyarara alisema linatarajia kutoa ajira za kudumu kwa Watanzania zaidi ya 300 na ajira za muda kwa watu zaidi ya 3000.

Naye Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko huo, Judith Kebara, alisema jengo hilo lina ghorofa 32 kwaajili ya makazi na biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ICON Hotel Group Africa, Fred Maina baada ya kusaini mkataba wa uendeshaji hoteli katika jengo la Mzizima Tower linalomilikiwa na NSSF. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NSSF, Abdi Kagomba. (Picha na Francis Dande).  
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati) akibadilishana hati na Philomon Tai. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati), akisaini hati na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ICON Hotel Group Africa, Fred Maina  wa uendeshaji wa hoteli katika jengo la Mzizima Tower linalomilikiwa na NSSF. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NSSF, Abdi Kagomba. 
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages