Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo, alitunuku jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo,akimtunuku Evelyn Wallace Shundi Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
Wahitimu Agnes Nsokolo (kulia) na Asha Kidendei wakiwa na furaha baada ya kuwa miongoni mwa wahitimu 43 waliotunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
Evelyn Shundi ambaye ni mfanyakazi wa Ewura akiwa na furaha wakati wa mahafali hayo.
Wahitimu wakivaa kofia baada ya kutukiwa
Mmoja wa wanafunzi akipatiwa cheti wakati wa mahafali hayo
Wakivaa kofia ikiwa ni ishara ya kunukiwa
Wahitimu wakiwa wamekaa baada ya kutunukiwa
Wahitimu wakiwa wamesimama mbele ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakisubiri kutunukiwa Shahada ya Uzamili
Domina Rwemanyila (kushoto) na Diana Tengia wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa Sahada ya Sanaa ya Mawasiliano ya Umma
Ni furaha iliyoje kutunukiwa Shahada ya Uzamili
Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Dk Frederick Shoo na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliotunukiwa Sahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara
Wapigapicha wakiwa kazini wakati wa mahafali hayo
Brass Band ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakipiga wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha mahafali hayo
Julieth (katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuhitimu katika chuo hicho.
No comments:
Post a Comment