HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 08, 2016

MKUTANO WA BARAZA KUU LA 24 LA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA WAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Profesa Faustin Kamuzora, akizungumza wakati alipokuwa akifunga mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa baraza hilo, Kaimu Postamasta Mkuu wa shirika, Fortunatus Kapinga na kushoto ni Kaimu Meneja Biashara wa shirika, Janeth Msofe. Kwa sasa Profesa Kamuzora amehamishiwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais. 
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 24 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, wakimsikiliza mgeni rasmi.
Katibu wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Meneja wa Posta Mkoa wa Iringa, Emmanuel Lugomera, akizungumza wakati wa kufungwa kwa mkutano huo. 
Mjumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, kutoka Pemba, Zanzibar, Mussa Bilal, akitoa neno la shukurani kwa Katibu Mkuu, Profesa Kamuzora. 
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika, Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment

Pages