HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 21, 2016

NSSF yawakumbuka yatima kituo cha Msimbazi Center


 Meneja Kiongozi wa NSSF Wilaya ya Ilala, Xavier Lukuvi (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Sabuni, Dawa za kufanyia usafi, Sista Anna Francis wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya sikukuu ya Krismas.
 Meneja Kiongozi wa NSSF Wilaya ya Ilala, Xavier Lukuvi (kushoto), akimkabidhi risiti ya malipo ya Umeme, Sista Anna Francis wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa NSSF wakiwa na Sista Anna. 
 Mmoja wa Maofisa wa NSSF akiwa amebeba mtoto.
 Watoto wanaolelea katika kituo cha Msimbazi Center wakicheza katika kituo hicho. 
 Watoto wakiwa na walezi wao.
 Sista Anna akipokea msaada wa vyakula, mafuta, sabuni.
 Meneja Kiongozi wa NSSF Wilaya ya Ilala, Xavier Lukuvi (kushoto), akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Shs. Milioni 1.6,  Sista Anna Francis wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Center jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Sikukuu ya Krisimasi. 

NA MWANDISHI WETU

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa msaada kwa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Msimbazi Center. Msaada huo ni mwendelezo wa NSSF katika kurudisha faida kwa jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Kiongozi wa NSSF Wilaya ya Ilala, Xavier Lukuvi, alisema kwamba lengo la msaada huo ni kusaidia kuboresha huduma katika kituo hicho pamoja na kufurahia sherehe za krismasi na mwaka mpya.

Alisema wametoa vyakula na kadi ya umeme ikiwa ni kuwakumbuka watoto hao na kuwaonyesha kwamba wako pamoja na NSSF inawapenda na kuwajali.

"Tunaendelea kuimarisha ujirani kwa kuwakumbuka watoto yatima ambao ni jukumu letu sisi kuwasaidia, kuwapenda na kuwalea na hata kuwa sehemu ya maisha yetu," alisema Lukuvi.

Naye Mlezi wa kituo cha Msimbazi Center, Sister Anna Francis, aliishukuru NSSF kwa msaada huo kwa watoto.
“Mungu awabariki mzidi kutoa, kutoa si utajiri bali ni moyo, tunawashukuru sana NSSF na uongozi mzima kwa kutukumbuka kwa zawadi ya vyakula na kadi ya umeme huu ni mchango mkubwa sana kwa watoto na wamefurahi,”alisema

Aidha aliziomba taasisi zingine kuiga mfano wa NSSF kuijali jamii na wasiojiweza.

No comments:

Post a Comment

Pages