Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika kutekeleza sera yake ya kurudisha fadhili kwa jamii imeendelea kusaidia katika nyanja mbalimbali.
Shirika hilo limetoa msaada wa kuisaidia taasisi inayoshughulika mambo ya Afya, Ukimwa ya Benjamin Mkapa Foundation, NSSF limetoa msaada huo ikiwa kama sehemu ya kuijali jamii katika masuala mazima ya afya ambapo msaada huo ulipelekwa moja kwa moja katika taasisi hiyo.
Msemaji wa NSSF, Salim Kimaro alisema kuwa msaada huo utaleta tija na kulitangaza Shirika kwa kuwa NSSF linatoa mafao ya matibabu na hivyo imeona iungane na taasisi ya Benjamin Mkapa inayoshughulika na masuala ya matibabu katika suala zima la kufanya afya za watanzania kuwa bora zaidi.
Hata hivyo msaada huo ulitumika katika ujenzi wa maabara pamoja na nyumba za wafanyakazi wanaoshughulika na masuala ya afya.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu ambapo aliwashukuru NSSF na taasisi zingine zilizofanikisha ujenzi huo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Majengo ya Maabara pamoja na nyumba za wafanyakazi wanaoshughulikia na masuala ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), imechangia ujenzi huo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikagua maabara hiyo.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment