NA KENNETH NGELESI, MBEYA
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa katika jaribio la kutaka kuiba kwenye duka la soda na bia za jumla ambaye pia ni wakala wa M-Pesa mali ya Mwandapile.
Tukio hilo limetokea Disemba 19 mwaka huu majira ya saa 1:45 jioni Kijiji cha Busisya, Kata ya Kisiba, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi iliyosaniwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhairi Kidavashari inaeleza kuwa Askari Polisi Mbeya Mjini kwa kushirikiana na Askari Polisi Wilaya ya Rungwe kwa pamoja walipata taarifa za siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha ambao walikuwa na lengo la kufanya uvamizi katika Duka hilo.
Baada ya taarifa hiyo Polisi walianza kuwa fatilia na hatimaye majira ya saa 1:45 askari walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki aina ya T- Better ambayo haina namba ya usajili yenye rangi nyekundu.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa na baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari walianza kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi hao.
Askari walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo hapo na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.
Aidha katika tukio hilo silaha bunduki tatu pamoja na risasi tisa ziliweza kupatikana zilizokuwa zinatumiwa na majambazi hayo. Silaha hizo ni Mark IV yenye namba 38482 na risasi mbili, Shirt Gun Greener yenye namba G.73878 na risasi 01 na Gobole lililotengenezwa kienyeji ambalo halina namba na risasi 06.
Aidha baada ya kupekuliwa majambazi hao walikutwa na vitu vingine ambavyo ni Rungu moja, Praizi moja, Bisibisi moja, mafuta ya cherehani, koti la ngozi rangi ya brown pamoja na begi dogo rangi nyeusi ambalo lilitumika kuhifadhi vitu hivyo.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Serikali Makandana Wilaya ya Rungwe kwa uchunguzi wa kitabibu na bado haijatambulika. Na kwamba mapaka sasa Msako bado ununaendelea na katika tukio hilo hakuna mali iliyoporwa wala askari kupata madhara.
No comments:
Post a Comment