HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 13, 2016

WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 55 YA UHURU WAKABIDHIWA VYETI


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara ,kiongozi wa msafara wa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru akivishwa shada la maua mara baada ya kufika katika lango la Marangu. 
Meneja wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adeventure,Rahma Adam akisalimiana na Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika lango la Marangu.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Washiriki wa zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kufika katika lango la Marangu zilipo ofisi za KINAPA.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamanda wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Mstaafu Jenerali George Waitara akiznungumza mara baada ya kushuka Mlima Kilimanjaro ambako timu ya Watu 36 wakiwemo Askari wa jeshi la Wananchi na Waaandishi wa Habari wamepanda mlima huo kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na askari wa jeshi la ulinzi waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waongoza watalii walioshiriki kufanikisha safari ya Waandishi wa Habari na Askari wa jeshi la Ulinzi  kupanda mlima Kilimanjaro.    Na Dixon Busagaga wa Blogu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Pages