HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 25, 2017

TCCIA INVESTMENT PLC YAZINDUA UUZAJI HISA DSE


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TCCIA Investment, Donald Kamori akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Uuzaji wa Hisa za Kampuni ya TCCIA  Investment katika hafla iliyofanyika jijini leo Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa uzinduzi wa Uuzaji wa Hisa za Kampuni ya TCCIA  Investment katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya washiriki.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya EAG Group, Imani Kajula akiwa na Humphrey Kibonde.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji TCCIA, Prof. Lucian Msambichaka akizungumza katika hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika (wa pili kushoto), akipeana mkono na  Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji Kampuni ya TCCIA, Prof. Lucian Msambichaka.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika (katikati), pamoja na viongozi wa Kampuni ya TCCIA Investment wakionesha kitabu cha mwongozo wa jinsi mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la DSE. 
Mgeni rasmi akipata maelezo baada ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja.
Mshereheshaji wa hafla hiyo, Humphrey Kibonde (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa EAG Group, Imani Kajula.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dorothy Mwanyika (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Uuzaji wa Hisa za Kampuni ya TCCIA  Investment katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TCCIA Investment, Aloys Mwamanga, Ofisa Mtendaji Mkuu TCCIA Investment, Donald Kamori na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji TCCIA, Prof. Lucian Msambichaka.

Dar es Salaam, Tanzania


NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dorothy Mwanyika amesema uchumi wa nchi utaweza kupaa zaidi ikiwa kutakuwepo na nguvu kazi yenye elimu na weledi wa kutosha.
Mwanyika aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati akizindua uuzwaji wa hisa za kampuni ya TCCIA Investment PLC katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).
Alisema ili kuweza kufanikiwa kiuchumi katika taifa lolote ni lazima wananchi wakawa na elimu ya kutosha, ambapo aliushauri uongozi wa TCCIA Investment kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu(HELSB) na benki kuwezesha wanafunzi wengi zaidi kupata mikopo.
“Najua kabisa kuna wazazi wengi ambao wangefurahi na kuwa tayari kuchukua mikopo maalum ya kusomesha watoto wao vyuo vikuu, hii ni fursa nzuri kwenu ikiwa mtaweza kushirikiana na benki pamoja na bodi ya mikopo kwenye eneo hili” alisema Mwanyika.
Akizungumzia uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya uwekezaji kwa njia ya hisa alisema ni kweli kwamba wananchi wengi wana uelewa mdogo na kuongeza kwamba hali hiyo itaendelea kuathiri ushiriki wao katika kutumia fursa zinazotengenezwa endapo itashindwa kutatuliwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCCIA Aloys Mwamanga alisema wanatarajia kuuza hisa zenye thamani ya Sh. Bilioni 45 ambapo fedha zitakazopatikana kama sehemu ya faida zitatumika kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ikiwamo kuwekeza kwenye viwanda vya kuchakata mazao.
Pia alitoa wito kwa wananchi kununua hisa za kampuni hiyo ambazo zinatarajia kuanza kuuzwa Februari 1 katika soko la hisa la DSE.Ã¥

No comments:

Post a Comment

Pages