NA
MWANDISHI WETU
MTANZANIA Alphonce Felix Simbu ameibuka kidedea baada ya
kukamata namba moja katika mbio za kimataifa za Standard Chartered Mumbai
Marathon zilizofanyika nchini India, jana.
Simbu ambaye ni Balozi wa DSTv, aliibuka mshindi akitumia saa
2:09.32 na kuwabwaga Wakenya na Waethiopia katika kumi bora.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Joshua Kipkorir aliyetumia saa
2:09.50 akifuatiwa na Eliud Barngetuny 2:10.39 huku nafasi ya nne ikichukuliwa
na Jacob Cesari saa 2:11.36 wote kutoka Kenya na wa tano ni Bonsa Dida saa
2:11.55 Ethiopia.
Mshindi wa sita aliibuka Samuel Mwanki wa Ethiopia saa
2:12.26 akifuatiwa na mwenzake Seboka Dibaba saa 2:12.37, nafasi ya nane
ikaenda kwa Levy Matebo saa 2.13:05 wa tisa ni Alex Saekwo 2:13.16 huku kumi
bora ikifungwa na Alfonce Kigen 2:13.42 wote kutoka Kenya.
Pia mtanzania mwingine kwa upande wa wanawake, Magdalena Crisprin alishika nafasi
ya nne akitumia saa 2:34.51.
Mbio zinatambuliwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa
(IAAF), na kuthibitishwa na ‘Association of International Marathon and Road
Race’ (AIMS).
Kwa upande wa Kocha wake, Francis John, alisema mafanikio ya
Simbu ambaye katika michezo ya Olimpiki Rio Agosti mwaka jana alishika nafasi
ya tano, ni matunda ya kambi ya zaidi ya miezi sita iliyowekwa na RT West
Kilimanjaro, Siha mkoani Kilimanjaro mwaka jana wakati wa kujiandaa na
Olimpiki.
Akizungumzia ushindi huo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT), alisema Simbu ana nidhamu ya mazoezi, mawasiliano mazuri na
shirikisho na ndio chachu ya kufanya kwake vizuri.
Gidabuday, alisema wakati wanampa ruhusa ya kwenda kushiriki
mbio walimuasa kwamba akakimbie kwa akili zaidi badala ya nguvu apate muda
mzuri.
MTANZANIA Alphonce Felix Simbu (wa pili kushoto) akiwa na washindi wenzake.
Simbu ambaye ni Balozi wa DSTv, aliibuka mshindi akitumia saa 2:09.32 na kuwabwaga Wakenya na Waethiopia katika kumi bora.
Simbu.
MTANZANIA Alphonce Felix Simbu (wa tatu kushoto) akiwa na washindi wenzake pamoja na askari wa India.
No comments:
Post a Comment