January 28, 2017

UB MBIONI KUANZISHA KOZI YA MAADILI

Na Happiness Katabazi ( UB) 

CHUO Kikuu cha Bagamoyo ( UB) , kimesema kipo mbioni kuanzisha Taasisi ya Maadili chuoni hapo  ambayo taaisis hiyo itaanzisha  kozi ya Maadili ambayo kila mwanafunzi bila kujali fani atalazimika kuisoma kozi hiyo . 

Hayo yamesemwa Leo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu, Profesa Costa Mahalu Katika sherehe ya kukabidhi wanafunzi ambao washindi wa shindano la kuandika Insha liloandaliwa na  Taasisi ya kiraia toka nchini Kenya ya Fahamu Ikishirikiana  na UB Iliyofanyika Katika madarasa ya chuo hicho Kawe Beach Dar Es Salaam Leo  kuhudhuriwa  na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho,Jaji Mstaafu wa   Mahakama ya Rufani, Dk.Stephen Bwana.

Profesa Mahalu alisema suala la Maadili Katika Jamii ni zito na Hakuna ubishi kwamba Jamii yetu pia inakabiliwa na tatizo la mmomonyoko wa Maadili hivyo UB Imeona ni vyema siku za usoni ianzishe Taasisi ya Maadili ambayo itakuwa na masomo ambayo yatafundishwa kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusu suala zima la Maadili kwa wasomi hao wa fani mbalimbali.

" Wakati tunaanzisha  UB  mwaka 2011 ,waasisi wa UB tuliona Kuwa UB iwe na somo la " Leadership and Good Governance' , kwasababu tulikuwa tunafahahamu  Nchi za Afrika  bado zinakabiliwa na tatizo la viongozi bora  , hivyo tukaanzisha somo Hilo ambalo nilazima mwanafunzi anayesoma UB wa ngazi yoyote asome hilo somo ambalo linamsaidia mwanafunzi  kutambua kiongozi mahali popote pale aweje,mambo gani afanye na yapi asifanye .

Alisema Tayari  mchakato wa  kuanzisha Taasisi hiyo unaendelea  na upo  Katika Hatua nzuri na Pindi utakapokamilika ,wataufahamisha  umma na Jamii ya wasomi wa chuo hicho.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Kozi ya 'Leadership and Good Governance ' , Dk.Asia Mwanzi alisema Lengo la mashindano hayo  yaliyofadhiliwa na Taasisi ya FAHAMU ni kuwajengea wanafunzi wa chuo hicho uwezo wa kukaa  chini na kuandika mambo mbalimbali yanayohusu Jamii Yao bila woga ili mamlaka husika Iweze kuyafanyiakazi  mawazo Yao .

Akizungumza baada ya kukabidhiwa na Jaji  Mstaafu Dk.Bwana Tuzo ,Dola Mia Moja za Kimarekani, vitabu  mshindi wa kwanza ambaye ni Mwanafunzi Baraka Samuel alisema amefurahishwa na ushindi huo Kwani washiriki walikuwa ni Wengi lakini Insha yake ikaibuka Kuwa mshindi.

Baraka alisema Insha yake Ameandika kuhusu sera Taasisi ya Vyuo Vikuu ( TCU)   ya kuinua viwango ya kudahili wanafunzi wanaojiunga  kujiunga na Vyuo vikuu nchini ambapo ameshauri TCU na serikali kwanza iboreshe elimu za Msingi na Sekondari ikishafanikiwa Katika ngazi hizo ndiyo ije iongeze viwango Vya udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu.

Mshindi wa pili ni Mwanafunzi wa Shahada ya pili ya Sheria ambaye pia ni Wakili wa Serikali ,Frola Massawe ambaye naye amepewa Tuzo.

Imetolewa na Ofisa Habari wa UB 
Happiness Katabazi
28/1/2017.

No comments:

Post a Comment

Pages