HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2017

Mbowe amgome Makonda

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo kuhusu sakata la kuhusishwa na tuhuma za biashara ya dawa za kulevya zinazomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu wito wa kumtaka kuripoti Kituo Kikuu Polisi baada ya kuhusishwa na tuhuma za  biashara ya dawa za kulevya. 
 Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu wito wa kumtaka kuripoti Kituo Kikuu Polisi baada ya kuhusishwa na tuhuma za  biashara ya dawa za kulevya. 

NA IBRAHIM YAMOLA, DODOMA

KIONGOZI wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fremaan Mbowe amesema, hawezi kwenda kuripoti Polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema kitendo alichokifanya Makonda cha kumhusisha kwa namna moja au nyingine na sakata la dawa za kulevya hatolikubali na atamfungulia kesi mahakamani.

Mbowe amesema iwapo Jeshi la Polisi litamwita atakuwa tayari kwenda siku na wakati wowote na kutoa ushirikiano woto watakaoutaka lakini si agizo la Mkuu wa Mkoa, Makonda.

Jumatano hii, Makonda alitaja majina 65 ya watu aliodai kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na dawa za kulevya akiwamo Mbowe huku akiwataka kuripoti Kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jana kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo, jana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma, Mbowe alisema: “Ninakanusha, kwa nguvu zote kuhusika kwa njia zote kufanya biashara au kutumia dawa za kulevya kutumia dawa za kulevua…mimi ni mtu mzima, ni kiongozi wa mda mrefu, sijawahi kujihusisha kwa njia yoyote na dawa za kulevya.”

“RC wa Dar es Salaam siyo Polisi na kwa mjibu wa Sheria hana mamlaka ya kuwataka watu kwenda polisi, Watanzania wameonewa kwa muda mrefu sana na viongozi hawa wamejipa mamlaka sana na mimi sitokwenda ng’o kwa amari ya Makonda ila Polisi wakinitaka nitakwenda,” aliongeza:

Akizungumza kwa msisitizo, Mbowe alisema: “Mkuu wa mkoa hana mamlaka na hajapewa mamlaka hayo ya kuwataka watu waende kituo cha polisi, anawaonea watu anajiona ana mamlaka makubwa anapoona amezungukwa na askari.”

Alisema nchi inaongozwa kwa Katiba, Sheria na Kanuni mbalimbali na unapotaka kutegereza jambo lina kanuni lakini ikiruhusiwa kufanyika kama anavyofanya Makonda nchi itaanguka.

“Tumeona kosa hili linafanya na Rais na sasa limeingizwa na wakuu wa mkoa na wilaya, sasa masuala ya jinai yana utaratibu wake na kipekee makosa yanayohusu dawa za kulevya yana sheria yake na yana vyombo mahususi ya kushughulikia, RC hana mamlaka ya kuchunguza dawa za kulevya na kimsingi ukiangalia mfumo wote, anawaepusha wafanyabishara wa dawa za kulevya, makosa ya dawa za kulevya hayana dhamana,” alisema Mbowe.

Katika mazungumza yake Mbowe alisema:“Jeshi la Polisi linaendesha kwa mjibu wa sheria na si matamko ya viogozi wa. Polisi wanatakiwa wafanye kazi kwa taratibu zao…siyo kila mtu anafanya ‘arrest’ ya mtu, wamefundishwa uchungizi, kuchungza mambo mbalimbali, hivi huyu Makonda ni nani, hajui kwamba anavuruga ushahidi na hivi kweli kuna mfanyabishara ambaye anauza unga amesikia kelele hizi atabaki nchini, anaharibu ushahidi huyu.”

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai alisema wao hakuna mtu anayepinga viti za dawa za kulevya, wanaunga mkono na wako tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa lakini utaratibu ufuatwe.

“Siogopo Polisi au siogopi mtu yoyote ila siwezi kukubali mjinga mmoja akaamua kutumia mamlaka yake kuchafua… hivi ana hela ya kumlipa Mbowe, mimi ni kiongozi wa chama, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, nina  familia,” alisema Mbowe

“Nitamshitaki Makonda ‘as a person’ na sitaishitaki Jamhuri, Makonda hana fedha ya kunilipa mimi, nina heshima yangu, siwezi kukubali mtu mmoja tena mbele ya vyombo vya habari anichafue, haya anayoyafanya Makonda ni sawa na utoto…ananiita mimi Polisi yeye kama nani, siwezi kwenda kwani hana mamlaka hayo na nitakuwa tayari kwenda pale nitakapoitwa na vyombo vinavyotambulika kusheria.”

Huku akiwaonesha kundi la wabunge wa upinzani kwa kusema: “Hawa  wote walioko nyuma yangu wanaongozwa na muuza dawa za kulevya…upumbavu huo siwezi kukubali, Makonda atabeba mzigo huo na sihitaji uchunguzi wa polisi kujua am innocent.”

Zitto: Ningekuwa punda wa Mbowe
Katika mkutano huo na waandishi uliohudhuliwa pia na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alisema: “Mimi ningekushangaa sana kama ungeenda polisi na umefanya uamuzi sahihi na kama wanakuhitaji wakupe wito wa kisheria lakini siyo mtu apite barabarani na karatasi za ajabu ajabu tu.”

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) alisema: “Mimi nimefanya kazi na Freeman, ameniibua nikiwa mtoto sana kutoka Chuo Kikuu, angekuwa ni mtu anahusika na dawa za kulevya mimi ningekuwa punda wake.”

Alisema anachokifanya Makonda ni kinyume na sheria kwani hana mamlaka hayo ya kuwataja watu kama alivyofanya na alichopaswa akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, ni kuliagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa hao aliowataja au kuwachunguza lakini si kuwataka waende polisi.

“Makonda atueleze anatumia Sheria gani kuwataka hao waliokwenda polisi…huyu Makonda alianza na wasanii leo amekuja kwa wanasiasa na hatujui ataendelea na nani lakini ni sheria gani anatumia,” alisema Zitto. Chanzo Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment

Pages