HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 10, 2017

SSRA YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WAPYA WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI (TUCTA)

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (kushoto), akishikana mikono pamoja na viongozi wapya wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakati wakiimba wimbo wao wa mshikamano katika semina ya kuwapatia elimu katika masuala ya Sekta ya hifadhi ya jamii, yakiwemo mafao, sheria na haki ya mfanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Rais wa Tucta, Tumaini Nyamuhokya na kulia ni Makamu wake, Quambos Sule. (Picha zote na Kassim Mbarouk).
Baadhi ya viongozi wa Tucta wakiimba wimbo wao wa mshikamano. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, akizungumza na viongozi hao, wakati akiwakaribisha katika semina hiyo, iliyoandaliwa na mamlaka hiyo. 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Dkt Yahya Msigwa, akizungumza wakati akiutambulisha ungozi wa shirikisho hilo katika semina hiyo, iliyondaliwa na SSRA, jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Quambos Sule, akizungumza wakati akielezea umuhimu wa Vyama vya wafanyakazi na Shirikisho hilo, kushirikishwa kwa karibu zaidi katika masuala mbalimbali ya kiutendaji na mamlaka hiyo, kwa kuwa SSRA ipo kwa ajili ya kusimamia maslahi ya wafanyakazi katika sekta ya hifadhi ya jamii.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamuhokya, akizungumza wakati akielezea kufurahishwa na SSRA kuwaita na kuwaandalia  semina hiyo, na kuelezea kuwa ameona ni jinsi gani mamlaka hiyo, inavyotambua umuhimu wa Vyama vya wafanyakazi katika masuala mbalimbali ya usimamizi na udhibiti wa sekta hiyo ya hifadhi ya jamii kwani ni katika masuala yanayowahusu wafanyakazi kijumla.
Baadhi ya wajmumbe na viongozi wa Tucta wakimsikiliza Rais wao, Tumaini Nyamuhokya. 
Baadhi ya Maofisa na Watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), wakifuatilia hotuba ya Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji cha SSRA, Sarah Kibonde.
Baadhi ya Maofisa wa SSRA wakiwa kazini katika kuandaa masuala mbalimbali ya semina hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, akiwasilisha mada kuhusu SSRA na Sekta ya Hifadhi ya Jamii. 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Dkt Yahya Msigwa, akizungumza kuhusu jinsi walivyoizipokea mada hizo, zilizowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SSRA, Irene Isaka.
Mwenyekiti wa semina hiyo, Rais wa Tucta, Tumaini Nyamuhokya, akiongoza semina hiyo katika kuingia kwenye majadiliano pamoja na ufafanuzi wa masuali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na wajumbe wa Tucta katika semina hiyo.
Mwakilishi wa Chama cha RAAWU katika Kamati ya Utendaji ya Tucta, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Francis Michel, akitaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali ikiwemo ya kuhusu sheria zinazotawala sekta ya hifadhi ya jamii.  
Mjumbe wa Tucta kutoka Chama cha Wafanyakazi cha TALGWU, Dk. Salma Abdi Chande, akiulizia masuala mbalimbali katika hifadhi ya jamii pamoja na mamlaka hiyo.  
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa SSRA, Onorius Njole, akitoa ufafanuzi wa masuala ya kisheria kwa viongozi hao wa Tucta. 
Mkurugenzi wa Utafiti wa SSRA, Asgar Mushi, akijibu masuala mbalimbali pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala yanayohusu Hifadhi ya Jamii pamoja na SSRA. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (kushoto), akijibu maswali ya wajumbe wa Tucta pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali.
Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji wa SSRA, Lightness Mauki, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha COTWU (T), Juliana Mpanduji, akielezea furaha yake kuhusu elimu waliyoipata kutokana na semina hiyo, iliyondaliwa na SSRA na kuelezea matumaini yake kwamba mamlaka hiyo, itakuwa ikiwaandalia semina kama hizo ili kuzidi kuwapatia elimu zaidi katika sekta za hifadhi ya Jamii nchini.
Mwenyekiti wa semina hiyo, Rais wa Tucta, Tumaini Nyamuhokya, akizungumza wakati akiifunga semina hiyo. 
Viongozi wa Tucta na SSRA, wakiimba wimbo wa mshikamano baada ya kufungwa semina hiyo. 
Wakurugenzi na Maofisa wa SSRA, wakiimba wimbo wa mshikamano.
Moja ya picha ya pamoja ya vingozi wa Tucta na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (katikati), wakati wa semina hiyo. 
Moja ya picha ya pamoja ya vingozi wa Tucta na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (katikati), wakati wa semina hiyo. 
Picha ya pamoja ya vingozi wa juu wa Tucta na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (katikati), pamoja na Wakurugenzi na Maofisa wa SSRA.

No comments:

Post a Comment

Pages