Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyemba akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu wa kozi fupi katika chuo cha michezo Malya hivi karibuni. (Picha na Habari vyote na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza).
Catherine Laurence, akisoma Risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake wakati wa mahafali ya kozi fupi chuo cha Michezo Malya.
Na Atley Kuni- Mwanza
Serikali imesema itakuwa bega kwa bega na Chuo
cha michezo Malya ili kuhakikisha chuo hicho kinakuwa kitovu cha kuzalisha
walimu bora na wenye weledi katika masuala mazima ya michezo hapa nchini na
hata nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe, alipokuwa
akifunga mafuzo ya muda mfupi yanayo tolewa na chuo hicho, ambapo jumla ya
wahitimu wapatao sitini na tisa (69) walitunukiwa vyeti na waziri huyo.
Mwakyembe amesema, kama wizara, nilazima
wakifanye chuo cha Michezo Malya kuwa “Strategic thinking” kwa maana ya
stratejia ya wavumbuzi wa vipaji vya watu wa kada mbali mbali hususan katika
suala zima la walimu wa michezo “Nilipo tembelea na kukiona chuo nimepata picha
kamili ya chuo hiki, hii sasa inanipa shauku yakuwashauri muandae dira endelevu
kwa chuo chetu” alisema Mwakyembe.
Mwakyembe, amesema katika Ibara ya 161 (G) ya
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015-2020, inaweka bayana na kutia msukumo wa
masuala ya michezo, lakini pia Rais wa Jamhuri ya Muungano ameonesha dhamira ya
dhati katika hilo hata mbele ya Mataifa mengine ndio sababu Morocco, wanataka
kujenga ‘Sport Complex’ Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, amesema
katika kuhakikisha chuo hicho kinafanya vema katika siku za usoni wamedhamiria
kuongeza idadi ya kozi zitakazo kuwa inatolewa kwa wakurufunzi wanaotaka
kujiunga na chuo hicho ukiwepo mchezo wa Whushu ambapo China kupitia ujumbe wake
iliowakilishwa na Bi. Amber, uliozulu chuoni hapo wakati wa mahafali, umeonesha
nia yakuleta walimu wa Whushu.
Mbali na jukumu la kuongeza aina ya kozi
zitakazo tolewa na chuo hicho kwa ngazi ya Stashahada (Diploma) mkuu huyo
amemweleza waziri changamoto zinazo kikabili chuo hicho ambazo nipamoja na
uhaba wa maji, Gym ya mazoezi, hali inayosababisha timu mbali mbali za mpira wa
miguu zinazo tamani kwenda kuweka kambi katika eneo hilo kushindwa kutokana na
ukosefu wa Gym, “Mh. Waziri ilikuja timu ya Mbao FC, kilio chao kikubwa ilikuwa
ni eneo la Mazoezi ya viungo (Gym Fitness centre)” alisema mkuu huyo wa
chuo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Michezo
nchini Dkt. Yusuph Singo Omary, kutoka Wizara ya habari, amesema hivi sasa
Serikali ipo katika mchakato wa kutenga shule 55 ikiwa ni hatua itakayo saidia
katika kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo nchini kuanzia vijana
wanapokuwa wadogo.
Awali akimkaribisha Waziri wa habarikuzungumza
katika mahafali hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mtemi Msafiri,
alimuomba waziri, Wizara ya habari kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na
TAMISEMI, kuona Umuhimu wakukisaidia chuo hicho katika kukiendeleza, “Tunaomba
Mhe. Waziri ili chuo hiki kiweze kwenda mbele basi vema kila Halmashauri
ikaagizwa kugharamia angalau Walimu wawili kila mwaka”, alisema Msafiri na
kuongeza kuwa endapo Halmashauri zote nchini 189, zikileta walimu wawili tu
basi tutakuwa na wanafunzi 378, hii itakisaidia chuo chetu kukua zaidi, lakini
pia kupata walimu wenye weledi.
Kwa upande wao wahitimu hao wamemuomba waziri
kupewa kipaumbele katika Michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA, Akisoma Risala kwa
niaba ya wahitimu wenzake Catherine Laurent, amesema wao wamejifunza Sheria na
kanuni za Michezo mbali mbali kwa kipindi chote walichokuwepo chuoni hapo hivyo
wanaomba kupewa kipaumbele katika kufundisha michezo pindi warejeapo kwenye
vituo vyao vya kazi kwani sasa wanatambua sheria, kanuni na taratibu zinazo
ongoza michezo waliyo jifunza.
Chuo cha michezo Malya kilianzishwa mwaka 1979,
kikiwa na lengo la kufundisha na uendeleza walimu wa michezo katika ngazi ya
Astashahada na badae mwaka 1995, ndipo kilianza kuzalisha walimu wanafunzi wa
ngazi ya Stashahada (Diploma). Lakini pia kimekuwa kikiendesha kozi fupi za
wiki mbili ambazo huwajengea uwezo wahusika kabla yakuendelea na ngazi ya
Diploma.
No comments:
Post a Comment