Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya wachambuzi wa soka wamesema kuwa kutokana na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana ikawa ndiyo nafasi kwa yanga kutetea ubingwa wao ambapo baada ya mchezo wa leo Simba wamebaki na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita kileleni wakiwa na pointi 56 baada ya michezo 25.
katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1 ambapo mabao ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph Huku bao la pili likifungwa na Edward Christopher huku bao la kufutia machozi kwa Simba sports Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili.
Kwa matokoe hayo yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiw ana Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 huku nafasi ya nne ikishikwa na Azam wenye pointi 44.Zacharia Hans Poppe akiwa hana hamu baada ya kushuhudia Timu ya Simba ikinyukwa bao 2-1 na Timu ya Wanankurukumbi Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kagera Sugar leo hii jumapili.
Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime akisalimiana na Mayanja wa Simba leo muda mfupi kabla ya mtanange kuanza.
Mashabiki waliingia kwa wingi kwenye Mtanange huo ulikuwa na hamsha hamsha ya kila aina yake.
Kikosi cha Simba kilichoanza
Mashabiki wa timu ya Kagera Sugar wakiwa jukwaa kuu kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar kuanza.
Kikosi cha Kagera Sugar kikiomba kabla ya mtanange kuanza
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi Simba ya Jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Mbaraka Yusuph
Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haamini kilichotokea baada ya timu yake kufungwa bao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu bara uliopigwa uwnaja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mbaraka akipongezwa kwa bao
Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog
Kocha mkuu wa Simba Mcameroon Joseph Omog akiwa haaminiTimu yake ikiwa nyuma ya bao 2-0.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakishangilia.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Mrundi Laudit Mavugo akijaribu kumtoka Beki wa Kagera Sugar Juma Ramadhan .
Kichuya Akiambaa na Mpira
Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude akitafakari baada ya timu yake kuchapwa bao 2-1 na Kagera Sugar.Winga wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiambaa na mpira wakati mchezo ukiendelea
Kiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Meza kuu
Mecky Mexime Kocha wa Kagera Sugar akiwa amebebwa na Wachezaji wa Kagera mara baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.
Simba walipata bao lao la pekee kipindi cha pili dakika ya 61 na mtanange kuwa 2-1
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa pamoja na Mlinda mlango wao Juma Kaseja.
Mtanange ulipomalizika Kipa Kaseja alipewa zawadi na Mashabiki wa Kagera Sugar pamoja na Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
No comments:
Post a Comment