HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 11, 2017

Makampuni ya simu yaungana kutoa huduma zaz kifedha

Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce akitoa elimu kwa mmoja wa watumiaji wamitandano ya simu kwa namna Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile ile.

Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile ile. 

Kwenye muungano huo ambao unaitwa Taifa Moja, makampuni matatu makubwa ya kutoa huduma za simu za mkononi ya Tigo Tanzania, Airtel Tanzania na Zantel, wateja wanaweza kutuma pesa na kupokea kutoka kwenye moja ya mitandao hiyo kwa gharama zile zile.

 Hapo awali, kutuma pesa au kupokea pesa kutoka mtandao tofauti mteja alikuwa akipokea ujumbe mfupi ambao ilikuwa ni lazima apeleke kwa wakala wa mtandao ambao amepokea fedha kutoka na ilikuwa izizidi siku saba tofauti na hapo fedha hiyo ilikuwa inarudi kwa aliyetuma. 

Kwa huduma hii, mteja anapaswa kuchangia huduma ya kutuma pesa kutoka kwa menu ya kawaida, halafu anachangua kutuma pesa kwenda mitando mingine. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutembelea watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa, Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce alisema kupitia muungano wa Taifa Moja wameweza kuwafanya wateja wapate njia rahisi ya kutuma na kupokea fedha.

Tunajua hapo zamani kuna baadhi ya wateja walikuwa wanapata wakati mgumu linapokuja suala la kutuma na kupokea fedha. Ilikuwa aidha upokee fedha kwa ujumbe mfupi au uwe na laini ya simu zaidi ya moja. Ukipokea fedha kwa ujumbe na kwa bahati mbaya ukaufuta ilikuwa inamaanisha fedha imepotea, alisema Alphonce. 

Lakini vile vile si kila mtu anayepokea fedha kupitia simu ya mkononi anahitataji kutoa. Wengine wanataka kulipia huduma mbali mbali kupitia huduma ya simu kama kulipia maji, kununua umeme au matumizi mengineyo. Kwa huduma hii mpya ya Taifa Moja imekuwa ni njia rahisi kwa wateja wetu, aliongeza Alphonce 

Kupitia huduma hii ya kutuma pesa na kupokea kutoka mitandao yeyote itachangia kuongeza idadi ya watu wanaotumia huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia simu za mkononi na pia kuongeza faida kwa makampuni ya simu. 

Hii ni mara ya kwanza Tanzania kwa makampuni ya simu kuungana pamoja kwa huduma ya pamoja. Hata hivyo, Taifa Moja sio huduma au mtandao mpya mbali ni njia ambayo imepewa promosheni hii ya kutuma na kupokea fedha kutoka mtandao wowote. 

Kwa upande wake, Mkuu wa usambazaji mkoa wa Dar es Salaam kutoka kampuni ya Tigo Tanzania Lloyd Kaaya. alisema ni furaha kwao kuona kwamba wateja wa simu za mkononi kwa sasa hivi anaweza kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote kwa gharama zile zile. Hii inaamanisha matumizi wa kutuma pesa yataongeza na yatakuwa na manufaa kwa upande wetu, alisema Kaaya.

No comments:

Post a Comment

Pages