NA SALUM MKANDEMBA
BENKI ya NMB imezindua rasmi huduma ya NMB Wakala, huku ikiwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kuwa mawakala ili kutanua wigo wa ongezeko la wateja katika sehemu zao za biashara na kukuza pato lao.
Uzinduzi huo ulifanyika jana Makao Makuu ya NMB Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam, ambako Meneja wa Wakala wa Benki ya NMB, James Manyama, alisema NMB Wakala ni huduma ya Haraka, Nafuu na Salama kwa watumiaji.
Alibainishaa kuwa, kupitia NMB Wakala, wateja na wasio wateja wa NMB, wanaweza kufanya miamalaa mbalimbali ya malipo, ikiwemo kulipia huduma za LUKU, Ving’amuzi, TRA, Leseni, Ada za Shule, Bili za Maji pamoja na kutoa au kuweka fedha.
Manyama alisema kuwa, huduma hiyo inakuja kumaliza tatizo la matumizi ya muda, gharama na upotevu wa fedha, na kwamba NMB Wakala ni muendelezo wa kaulimbiu ya benki ya Karibu Yako, kwani inakwenda karibu zaidi na jamii.
“Tuna matawi 189, ATM zaidi ya 700 na mawakala zaidi ya 2,200, nchini kote, lakini hii haitufanyi kutopokea maombi mapya ya uwakala na ndio maana tunawaomba wenye sifa kujitokeza kuupata uwakala, ili kuongeza idadi ya wateja sehemu zao za biashara,” alisema.
Alizitaja sifa za kuomba NMB Wakala kuwa ni pamoja na mtaji wa usiopungua Sh. Mil 2, leseni ya iashara, uzoefu wa iaka miwili katika huduma za fedha, ofisi zisizo hamishika, pamoja na taratibu nyingine za ufunguzi wa biashara na dhamana.
Safi sana NMB...keep it up.
ReplyDelete