Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiwasili katika kikao kati yake na wazee Maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, kikilchofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Bw. Shaibu Bakari Ngatiche.
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wazee maarufu wa
Kata ya Mtama na Majengo A ,katika kikao chao kilichofanyika katika
ukumbi wa kaniasa la Katoliki,Mtama Lindi Vijijini.Mh Nape alizungumza
mambo mengi ikiwemo na kuwaomba Wana Mtama kusameheana kwa mambo yote
mabaya yaliyokuwa yametokea na kuanza ukurasa mpya wa kujenga undugu wa
kupendana na kushirikiana katika mampo mbalimbali,amewaomba kuziweka
kando itikadi zao za kisiasa na badala yake wakae kwa umoja wao wafirie
namna ya kuliletea maendeleo jimbo la Mtama.
"Ndugu zangu,Wazee Wangu siasa kwa sasa zimekwisha,niwaombe tu,itikadi zetu za kisiasa tulizokuwa nazo tuziweke kando,tuanze upya kwa pamoja kuijenga Mtama yetu ili ipige hatua katika suala zima la Maendeleo,na mie kwa vile nimepata nafasi ya kuhakikisha jimbo la Mtama linapata maendeleo,basi ntahakikisha yale yote niliyo yaahidi wakati wa kampeni,ndani ya miaka mitano niwe nimemaliza ama kuyakupunguza kwa kiasi kikubwa",alisema Nape.Picha na MichuziJr.
Baadhi
ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye
alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kuhakikisha jimbo la Mtama
na kusini kwa ujumla inaanza kupiga hatua kimaendeleo
Baadhi ya akina Mama waliofika kumsikiliza Mbunge wao
Mmoja wa Wananchi wa jimbo la Mtama akielezea moja ya changamoto ndani ya jimbo hilo,ambalo amemuomba Mh Nape alifanyie kazi
Mh.Nape akiwa katikati ya Wazee Maarufu wa jimbo la Mtama wakisubiri chakula cha pamoja
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Bw. Mohamed Nanyali akizungumza na
wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo
Mh. Nape Nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake kutoka maeneo
mbalimbali wakiwemo Wazee maarufu wa jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment